2017-02-23 16:40:00

Ishini vyema Ukristo wenu; acheni maisha ya undumilakuwili!


Kata mikono, na ng’oa jicho , lakini usiwakwaze wadogo, yaani wanye haki, wale ambao wanamtegemea Bwana, na rahisi kuamini Bwana.Ni wito wa Baba Mtakatifu Francisko asubuhi ya tarehe 23 Februari wakati wa Misa yake katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican akichambua sehemu ya Injili iliyosomwa ya siku akisema vikwazo kwa Bwana ni uharibifu.  Nini maana ya kikwazo, Baba Mtakatifu  anachambua juu ya hilo akisema ,kikwazo maana yake ni kusema jambo lakini ukafanya kinyume na hilo,au ni kuishi kwa sura mbili yaani mchanganyo ,kwani unasema mimi ni mkatoliki , ninakwenda kila siku kwenye misa, au niko katika chama fulani, lakini maisha yangu ni kitu tofauti na siyo maisha ya kikristo, kwa mfano siwalipi inavyo takiwa wafanyakazi wangu , ninawaonea na kuwanyonya watu , pia mimi ni mchafu katika biashara na fedha chafu.Baba Matakatifu anaongeza na wakatoliki wengi wako namna hiyo, kwa njia hiyo wanawakwaza wengine.

Je, ni mara ngapi tumesikia  wote wakitaja mtaa fulani na katika sehemu nyingine. Baba Mtakatifu anasema, kuwa  mkatoliki wa namna hiyo, bora ni kawa mpagani, kwasababu matendo ya namna hiyo ni vikwazo na yana haribu na kuangusha chini. Baba Mtakatifu anasema hayo mambo yanatokea kila siku, akitoa mfano, ya kwamba ukitaka kujua zaidi tazama matukio ya kwenye televisheni, taarifa za habari  na magazeti, kwani katika taarifa hizo kuna vikwazo vingi vilevile hata matangazo mengine ya biashara yanaleta  vikwazo katika na kuharibu jamii.

Akitoa mfano anasema, Kampuni moja muhimu ilikuwa hatihati ya kufilisika.Viongozi walitaka kuzuia watu wasifanye mgomo wa haki , lakini wasingefanya vizuri kwasababu wafanyakazi hao  walikuwa wanataka kuongea na viongozi  wa Kampuni hiyo.Watu hawa hawakuwa na fedha kwa ajili ya mahitaji yao ya kila siku kwasababu walikuwa hawapokei mshahara, lakini wakati huo huo Meneja mkatoliki wa Kampuni hiyo alikuwa likizo kipindi cha baridi huko mashariki ya mbali kwenye joto , watu walijua hata kama habari hiyo haikutokea katika magazeti, hiyo ndiyo vikwazo anaongeza Baba Mtakatifu.

Hata Yesu katika Injili alisema kwa wale  wanao toa vikwazo bila kusema kama ni vikwazo , lakini  wanajua , kwani watakapo bisha hodi wakisema ni mimi Bwana hunikumbuki, nilikuwa ninakwenda kanisani , nilikuwa karibu, nilikuwa mmojawapo wa chama fulani au nafanya haya na yale, hukumbuki sadaka nilizotoa ? Baba Mtakatifu anaongeza, ndiyo kumbukumbu  ya sadaka ya fedha chafu , zilizoibiwa kwa masikini, na hivyo sikutambui, ndilo jibu atakalo toa  Yesu kwa wale wanaoishi kwa vikwazo, maisha ya mchanganyo.

Kuishi mchanganyo unasabishwa na kufuata tamaa za moyo, yaani dhambi za mauti ambazo  ni majeraha ya dhambi ya asili, Baba Mtakatifu anasema, ndiyo maana somo la kwanza linatuonya kwanza  yakwamba tusipendelee kujikita katika utajiri , na pia kusema ninajitosheleza mwenyewe, hivyo ni mwaliko wa kutokuahirisha madiliko ya uongofu. Leo hii kila mmoja itakuwa vizuri kufikiria ndani ya maisha yake kama anaishi maisha mchanganyiko, wakati huo kwa kijujuu ukaonekama mwenye haki, na utadhani ni mwamini mwema , wakatoliki wazuri wakati chinichini wanafanya mchanganyo wa maisha . Itakuwa vizuri kutafakari kama kuna uaminifu wa kina , ukidhani kwamba Mungu atasamehe yote wakati ninaendelea na maovu yangu. Inabidi kujitafakari iwapo ninavyoishi siyo vizuri, ninahitaji mabadiliko na kuongoka leo hii bila kusubiri kesho.Jaribu kuchukulia kwa makini neno Bwana ambalo ni lenye ugumu sana , lakini vikwazo vinaharibu.

 

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.