2017-02-21 16:28:00

Kuhama ni suala la asili, ni mapito na marudio katika miongo


Napenda kuwashukuru na kwa utambuzi wa kazi nzuri mnayo itenda , kwa namna ya pekee shukrani kwa Askofu Mkuu Tomasi  kwa maneno yake ya hotuba na pia Dk Pottering naye kwa maneno  yake, vilevile usuhuda wa watu  watatu. Kwa dhati siyo rahisi kusoma changamoto za wakati wa sasa kuhusu  wahamiaji , na namna ya ujenzi wa amni , ukiwemo maendeleo endelevu, ambapo ilibidi kuanzisha hata Baraza la huduma ya maendeleo endelevu ya binadamu, na ndani yake kuwapo kitengo kimoja kinacho shughulika masuala ya wahamiaji ,wakimbizi na waathirika wa biashara ya binadamu. Ni maneno ya hotuba ya baba Mtakatifu Francisko alipokutana na wawakilishi wa Mkutano wa kimataifa kwa ajili ya wahamiaji na amani, Jumanne, 21 Februari 2017 mjini Vatican.

Katika matukio mbalimbali ya wahamiaji,  haiwakilishi kuwa ni matukio mapya katika historia ya binadamu.Bali matukio haya yameoneka kila muongo ambayo yamekuza makutano ya watu na kuundwa kwa ustaarabu mpya wa  jamii.Uwepo wa kuhama ni kielelezo kinacho leta furaha ya kila binadamu,hiyo ni furaha inayo paswa kutafutwa na kuifuata.Na zaidi kwa upande wa wakristo ,ambao wanao utambuzi wa dhati ya kuwa maisha yetu hapa duniani ni watembezi kuelekea makao yaliyo mema.

Mwanzo wa milenia hii ya tatu inasikika kwa nguvu na hasa kwenye sifa za harakati ya wanao hama.Kwa maana nyingine ni jambo la asili, ni mapito na pia  marudio ambayo yanagusa  kila kona ya dunia.Lakini kwa bahati mbaya katika sehemu nyingine, kesi hizi za wahamihaji, ni suala kulazimika kutokana na migogoro , majanga ya asili , mateso , mabadiliko ya tabia nchi, vurugu, umasikini ulio kithiri. Baba Mtakatifu anasema ,inastaajabisha idadi kubwa ya watu wanao hama kutoka bara moja kwenda bara nyingine, wakati huo unakuta pia wengine wana hama nchi yao na kusongamana katika sehemu moja lakini ni ndani ya nchi hiyo hiyo.Mtiririko wa sasa wa wahamiaji hata kama siyo wote lakini ni wenzi zaidi kuliko kipindi kilichopita.

Mbele ya matukio haya magumu Baba Mtakatifu anasema, anajisikia kueleza wasiwasi wake kwa wale wanao lazimishwa kuhama , kwa wakati huu na kufanya ongezeko la changamoto kubwa kwa  sera za kisiasa, jamii na Kanisa, ambao wanaitwa kujibu kwa haraka dharura ya hiyo kwa namna ya mpangilio unao stahili.Majibu ya dharura yanaweza kuzungukwa kwa maneno haya kukaribisha, kulinda , kuhamasisha na kukubalika. Baba Mtakatifu akielezea hayo maneno  anasema , ili kuweza kupokea au kukaribisha: kuna jambo ambalo linatuunganisha watu wote , kile kitendo cha kutokuangalia jirani kama vile ndugu yangu, na kumuacha hivyo au kupenda kumtawala tu bila kumkaribisha.Hiyo ni maana ya kumbagua , na kuonesha jinsi gani wewe ulivyo  mbinafsi.Baba Mtakatifu anasema inahitaji mabadiliko ili kushinda ule ubinafsi na woga,na badala yake  kuwa wakarimu na kuwapokea wale wanao bisha hodi milangoni kwetu.Ni wale wote wanao kimbia vita, na kushutukia wanaingia mikononi mwa maharamia. Inabidi kufungua milango ya kibinadamu yenye uwezekano wa kuwalinda.

 Neno kulinda:Baba Matakatifu mstaafu Benedikto wa VI alionesha uzoefu wa wahamiaji ya kwamba mara nyingi ni waathirika , ambao wana nyonywa , na kuteswa.Hivyo Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kusema hiyo ni kuongelea juu mamilioni ya wafanyakazi wahamiaji na miongoni mwao ni wale wasio na ajira, au  wanafanya kazi bila ruhusa yoyote, na hawapati riziki ya haki yao , hawa ni wahamiaji na wanaomba makazi, ni waathirika wa biashara ya utumwa.Kwa namna hiyo kuwalinda ndugu zetu ni jambo msingi na amri ya kimaadili katika kutafisiri kwenye vyombo vya kisheria , kitaifa na kimataifa , waote wanao husika , wanapaswa kufanya uchaguzi wa sera za kuona mbali , kuendelea kufanya michakato ya ujenzi japokuwa inafanyika polepole, lakini cha msingi mi kurudia makubalianio ya mara moja ya utekelezaji wa muungano katika kupambana na wafanya biashara wa  miili ya binadamu na kujitajirisha juu yao.Nijuhudi za wote  kama wadau na nguvu za kiserikali lakini daima hata Kanisa litakuwa karibu.Kuwalinda haki zao ni jambo muhimu ambapo ni kuhakikisha uhuru msingi na kujali utu wao , na hiyo ni zoezi ambalo siyo kukwepa . 

Kuhamasisha: Kulinda haitoshi , tunahitaji kukuza umuhimu wa binadamu wakimbizi , na wahamiaji , ambapo ni kufanya utekelezaji kwa njia ya huduma kwa ajili ya haki na amani na uadilifu wa viumbe katika maendeleo kwa mujibu wa mafundisho jamii ya Kanisa, ni haki isiyo kanushwa kwa kila binadamu, inabidi kuhakikisha usalama wa hali na mahitaji ya zoezi kama binafsi na jamii , katika usawa wa mambo msingi yanayo ruhusu uwezekano wa kuku ana kuchagua.Kwa njia hiyo hata katika kuhamasisha inahitajika nguvu ya pamoja , yaani sera za kisiasa ,jamii, mashirika ya kimatifa na taasisi za dini.Uhamasishaji wa binadamu kwa wahamihaji na familia zao, unaanzia katika jumuiya asili, mahali ambapo kuna uhakika, umoja na haki ya kuhama , hata haki ya kutokuweza kuhama, na haki ya kurudi makwao kwa hali ya kiutu .Kwa njia hiyo ni kuwatia moyo hasa sekta inayoshughulia masuala hayo ya mipango katika ushirikiano  wa kimataifa.

 Kukubalika au kuungana ,siyo kufananisha na wala kushirikiana , huo ni mchakato msingi juu ya kutambuana kila mmoja heshima kwa wengine na kuthamini utajiri wa utamaduni wa kila mmoja. Haina maana ya kuwa mwingine ni juu ya utamaduni wa wengine, na wala ile ya kubaguana kati yao , na kusababisha hatari ya kutenga mitaa ikawa mibovu . Jambo hili pia linawahusu wale wanao fika,lazima kuwa karibu na utamaduni na mila ya nchi na wenyeji wake kwa maana ya kuheshimu tamaduni za kila mmoja ikiwa ni pamoja na  kupokeana na kukubalika .Baba Mtakatifu anatoa wito akisisitiza juu ya sera za kisiasa katika kukuza namna ya kuunganisha familia.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.