2017-02-18 17:01:00

Mh. Pd. Oscar Nkolo Kanowa ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Mweka


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu Gèrard Mulumba Kalemba wa Jimbo Katoliki Mweka, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Mheshimiwa Padre Oscar Nkolo Kanowa kuwa Askofu mpya wa Jimbo katoliki la Mweka, nchini DRC. Kabla ya uteuzi huu Askofu mteule Oscar Nkolo Kanowa alikuwa ni mchumi wa nyumba ya malezi ya Mapadre wa "Scheut" eneo la Mbudi, Jimbo kuu la Kinshasa, DRC.

 

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.