2017-02-18 16:43:00

Kumbu kumbu ya Miaka 40 ya uhusiano wa Kidiplomasia Ghana na Vatican


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Kardinali Giuseppe Bertello, Rais wa Serikali ya mji wa Vatican, kuwa mwakilishi wake maalum katika kumbu kumbu ya maadhimisho ya Miaka 40 tangu Serikali ya Ghana ilipoanzisha uhusiano wa Kidiplomasia na Vatican, sanjari na kumbu kumbu ya miaka 60 tangu Ghana ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Mwingireza. Maadhimisho haya yataanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 3 Machi na kufikia kilele chake hapo tarehe 6 Machi 2017.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.