Zaidi ya waamini 250,000 kati yao wasio kuwa wakatoliki , wameshiriki sherehe ya miaka 100 ya uwepo wa madhabahu ya Mama Maria wa Lourdes Dantolingi Orissa nchini India siku chache zilizopita.Sehemu hiyo ni maarufu katika mji huo kwa kutembelewa na mahujaji wengi .Madhabahu hayo ya parokia yalitabarukiwa mwaka 1917 na wamisionari kutoka Ufaransa walio fika katika Serikali ya india kwa ajili ya kuwasaidia watu kutokana na baa la njaa na janga la mlipuko wa maradhi.
Habari kutoka katika gazeti la Osservatore Romano linasema Sherehe hizo zilianza kwa ngoma ya jadi ya kihindi na badaye ilifuata Ibada Takatifu ya Misa iliyo ongozwa na Askofu Mkuu John Barwa wa Jimbo Kuu la Cuttac-Bubaneswar akiwa na maaskofu wengine watano wa India,pamoja na mpadre 200, watawa 300 kutoka sehemu mbalimbali za nchi hiyo.Kwa upande wa familia moja isiyo katoliki ni Pratap Sahu na Mke wake Priti wanatoa ushuhuda wa muujiza walio upata, kwamba kwa miaka mingi waliishi bila kumpata mtoto, na baada ya kwenda kwenye madhabahu hiyo kuomba kwa mama Maria, wakafanikiwa mtoto.
Historia ya utamaduni wa Lourdes huko Orissa India, ilitokana na kipindi kigumu cha
ukame ulio kuwa umewakumba na kusabibisha vifo vya mamilioni ya watu huko India. Kwa
mwaka 1866 nchi ilipata baa la njaana kusababisha janga la kipindupindu na ndui iliyo
wauwa maelefu ya watu.Wakati wa Janga hilo ndipo wamisonari wa kwanza walifikia huko
wakiwa ni wa Shirika la Mtakatifu Francisko wa Sales.Wao walikusanya maelefu ya
watu waliokuwa wametengwa na pia watoto yatima na kuwakaribisha katika nyumba zao
huko Surada.Na pia huko Dantolingi, wamisionari walikusanya watu walio kuwa na ugonjwa
wa ndui na taratibu kuanza kuwapatia matibabu. Kwa maana hiyo mara baada ya janga
hili , wakazi wa sehemu hiyo waliomba wamisionari kujenga madhabahu ili wapate kumshukuru
Mama Maria kwa namana ya pekee kuwaokoa na njaa na balaa magonjwa ya mlipuko.
Padre Sanjeeb Kumara Beero Paroko wa Madhabahu hiyo anasisitiza kwamba kwa sasa
katika eneo hilo wanaishi takribani watu 250,000 ni familia ambazo taratibu zinazidi
kuongezeka.Kwa ushirikiano wa Parokia za Jimbo la Berhampur wanajaribi kuwasaidia
mahujaji wote wanahofika katika madhabahu hiyo.Anaongeza “ siyo kwamba mahujaji wanafika
mara moja kwa mwaka, bali wanafika mara moja kwa kila ijumaa ya mwezi , ambapo wao
wanalazimka kuandaa mafundisho ya kiroho na kuandaa vipindi vya sala.
Halikadhalika Askofu Aplinar wa Jimbo la Rayagada akiwa ni mwenyeji kutoka sehemu
hiyo ya Dantolingi anasema tunayo furaha kubwa kuona familia hizi zinajenga mshikamano
wa nguvu wa upendo na utulivu na watu wengine.
Aidha Askofu Sarat Chandra Nayak wa Jimbo la Berhampur anakumbuka mafundisho ya
familia yaliyoko katika wosia wa Baba Mtakatifu Juu ya familia furaha ya upendo na
pia juu ya wosia wa Furaha ya Injili akisema wosia huo unahusu kiini cha utume wa
Kanisa , namna ya kuinjilisha leo ulimwenguni, kwa kila hali na maendeleo yatakayo
jitokeza katika familia ,ni sawa sawa na maendeleo ya Kanisa kwa maana ulimwengu
mpya unaanza sasa akihusisha maisha ya ndoa, ambapo kwa namna ya pekee ndiyo mpango
wa shughuli za kichungaji kwa mwaka 2017 katika Jimbo lake.
Maadhimisho ya miaka 100 ya madhabu hayo yameanza kwa utangulizi wa siku tisa za sala,ambapo
kila siku ya maadhimisho ya sala , iliongozwa na mapadre mbalimbali na mada tofauti
kwa waamini zimeotolewa.
Sr Angela rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |