2017-02-15 16:15:00

Mahubiri ya Kwaresima 2017: Yesu ni Bwana!


Padre Raniero Cantalamessa mhubiri wa nyumba ya Kipapa wakati wa Kipindi cha Kwaresima kwa mwaka 2017 ataedesha Tafakari za Ijumaa kuanzia tarehe 10 Machi 2017; baadaye tarehe 17, 24 na 31 Machi 2017. Tafakari ya mwisho itatolewa tarehe 7 Aprili 2017. Kauli mbiu itakayoongoza tafakari za Kipindi cha Kwaresima zitakazotolewa na Padre Cantalamessa ni “Wala hawezi mtu kusema, “Yesu ni Bwana” Isipokuwa katika Roho Mtakatifu”. 1Kor. 12:3.

Huu ni mwendelezo wa tafakari zilizotolewa na Padre Cantalamessa kuhusu “Roho Mtakatifu” Nafsi ya Tatu katika Fumbo la Utatu Mtakatifu. Tafakari hizi zinalenga kuwasaidia waamini kuona jinsi ambavyo Roho Mtakatifu anavyowezesha kuufahamu ukweli wote mintarfu Fumbo la Pasaka, yaani mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu. Baba Mtakatifu Francisko, waandamizi wake wa karibu pamoja na wakuu wa Mashirika ya Kitawa na Kazi za kitume wanaalikwa kushiriki katika tafakari hizi zitakazokuwa zinaanza majira ya saa 3: 00 kwa saa za Ulaya.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.