2017-02-14 15:16:00

Makardinali: "Papa kanyaga twende tuko nyuma yako"!


Kardinali Oscar Andrès Rodriguez Maradiaga, Mratibu wa Baraza la Makardinari Washauri wa Baba Mtakatifu Francisko, katika kikao chao cha kumi na nane kinachohudhuriwa na Baba Mtakatifu mwenyewe, Jumatatu, tarehe 13 Februari 2017 amemhakikishia Baba Mtakatifu kwamba, Makardinali wanamuunga mkono na wanaridhia mchakato wa mageuzi anayoendelea kufanya kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Kanisa la Kristo Yesu ulimwenguni.

Kardinali Maradiaga amemshukuru na kumpongeza Baba Mtakatifu kwa hotuba yake ya salam na matashi mema kwa Sekretarieti kuu ya Vatican wakati wa maadhimisho ya Siku kuu ya Noeli kwa mwaka 2016 ambamo pamoja na mambo mengine alikazia umuhimu wa toba na wongofu wa ndani kama kiini cha mageuzi yanayofanywa kwa sasa mjini Vatican. Baba Mtakatifu anakaza kusema, haki ya kweli inafumbatwa katika upendo na huruma, ili kuweza kutekeleza mapenzi ya Mungu katika maisha ya mwanadamu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.