2017-02-14 14:29:00

13 Februari ni Siku ya Radio duniani ni chombo hai kuzidi kiasi


Jumatatu  13 Februari ilikuwa ni "Siku ya radio duniani" ikiwa na kauli mbiu "Radio ni wewe" ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO limetaka chombo hicho kitumiwe kuchagiza mashauriano. “Tunaishi katika mapinduzi ambamo tunabadilishana na kupata taarifa na bado katika mabadiliko haya, Radio imesalia kuwa muhimu na shirikishi”. Ni maneno ya Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova akitaka mapinduzi hayo sasa yachagize maendeleo endelevu.


Kila siku ni takaribani ya milioni 2,4 za watu duniani wana sikiliza radio Fm au kusikiliza kwa kupitia mitandao ya intaneti.Kwa sasa kuna aina nyingi za kusikiliza radio kadri miaka inavyozidi kupita ndivyo hata teknolojia, lugha inazidi kujionesha ukuaji wake na kupata mapinduzi na hata kujionesha kwenye teknolojia mpya ya digital. Naye Profesa wa historia ya Radio na Televisheni  katika Chuo Kikuu Katoliki cha Milan nchini Italia Giorgio Simonelli akihojiwa na mwandishi wa Habari wa Radio vatican anasema, Radio ni chombo kinacho unganisha tabia kuu mbili ambazo tunafanya utafiti, tabia ya kijamii na binafsi.Ni Radio ya  kijamii kwa sababu leo hii unaweza kusikia  radio unayo taka hata kama huko nchi ya Austraria, kwa maana hiyo ni kujenga jumuiya kubwa inayozunguka radio kwa njia ya kuchagua ambapo lakini ni uchaguzi binafsi. Zaidi Radio ni chombo nyenye nguvu na utambulisho, kwani kila msikilizaji wa radio akitaka kuonesha ni radio ipi anayosikiliza , jibu lake ni Radio yangu, hasemi televisheni yangu, kwa njia hiyo ni kuthibitisha juu ya kumiliki binafsi radio.


Akieleza juu ya kauli mbiu iliyochaguliwa na Unisco “Radio ni wewe”, anasema hili ni kama jina la kiini maacho, kwa ujumla matuminzi ya radio yamegunduliwa kwenye miaka kati ya 60 na 70 ikiwa na kanuni zake hafifu, maana walitoa mambo rahisi sana , lakini kwa wasikilizaji walijisikia kuhusika katika kuchagua nyimbo kama mtu alitaka kumtolea wimbo kwa heshima ya mwingine.Baadaye ikatokea mtindo mwingine kama vile 3131 ,lengo lilikuwa kumwezesha mtangazaji na msikilizaji waongee pamoja, maana kwanza  ilikuwa ni kutoa swali na baadaye mwingine kutoa mawazo yake kwa mjadala.Kwa upande wa watangazaji wamekuwa wazi kutoa nafasi kubwa kwa wasikilizaji wao katika mijadala mbalimbali.


Akifafanua zaidi juu ya matumizi ya Radio Profesa Simonelli anasema  mifano ya radio  kupitia mitandao, radio za vyuo vikuu vipindi  maalumu kwa ajili ya michezo, vimekuwa muhimu kwa wasikilizaji ,pia radio imekuwa daima huru kama chombo cha mawasiliano hat kutoa ripoti za matukio mengi ya kijamii yasiyo takiwa.Aidha  mfano kwa upande wa Afrika  Radio imesaidia sana katika kutoa taarifa muhimu za jamii, kwa mfano Stefano Leszczynski anatukumbusha mmisionari wa Kikomboniani  Padre Fabrizio Colombo mkurugenzi wa Signis wa Shirika lisilo la Kiserikali lenye kuwa na wanachama washiriki 140 ambapo wanashirikiana pamoja katika sekta ya Radio , televisheni, sinema , video , elimu juu ya mitandao , inteneti na teknolojia mpya ya mawasiliano.


Aidha anasema kwamba katika uzoefu wake wa radio zaidi katika Afrika,ameona  Radio ni jambo linalo jikita katika mioyo ya watu wengi , na jinsi gani radio inaweza kubadili hata maisha ya watu .Mfano kumhoji mtoto aliye nyanyaswa , anaweza kuleta mabadiliko ya jamii katika nchi.Anatoa mfano wa miongoni mwa mambo aliyo yaona Afrika kuhusu unyanyasaji wa watoto kama utumwa mamboleo,wazazi kuuza watoto wao, na kupotelea malishoni.Kwa njia ya mahojianao ya watoto walio toroka au kupata manyanyaso mara baada ya kukataa utii  na kwa njia ya historia hiyo kupitia radio, inaweza kuokoa watoto wengi walio kuwa wanakabiliwa na utumwa wa namna hiyo, hata kuiweka  serikali kuwa macho katika kukabiliana na utumwa na manyanyaso, hiyo ni mifano kuonesha jinsi gani Radio ni chombo kilicho hai na kati cha kuweza kubadili hata maisha.


Hali kadhalika radio imebadili mamilioni ya watu walio kuwa wanasikiliza radio vatican wakati wa vita vya Pili vya Dunia. Hasa ndugu wengi walio kuwa wamekimbia vurugu za vita.Katika studia  za Radio Vatican  kwa miaka 6 mfululizo waliweza kutuma ujumbe  1,200,000  ambao ni zaidi ya masaa 12,000 ya matangazo.
Kama leo hii tunatazama maendele endelevu, na  mabadiliko ni vema kumsikiliza kwa shahuku kubwa Papa Pio wa XI tarehe 12 Februari 1931 wakati anafanya uzinduzi  wa Radio mbele ya mwanzilishi wa Radio Vatican  Gugliermo Marconi akisema "Siri ya mpango wa Mungu  katika kufanikiwa kwa nafasi  ya  mitume mkuu ,kwa amri ya Mungu ili watu wote wapate kuhabarishwa kwa njia ya mafundisho na mahubiri kwa  kila kiumbe katika mataifa ,na hasa kuanzia kwanza  Marconi mahali ambapo tunaweza kufanya matumizi ya uvumbuzi wa ajabu"

 

Sr Angela Rwezula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.