Nchini Chad kumezuka ugonjwa wa Epatitis "E" ambao umeenea katika Mji wa Am Timan katika ukanda wa Mkoa wa Kusini Mashariki ya Salamat.Shirika la madakatari wa kutoa misaada ya kibinadamu wametoa taarifa hiyo ambapo tayari walikuwa wamegundua kesi ya kwanza Septemba 2016 .Tangu wakati huo Shirika hilo lisilo kuwa la kiserikali limepata kutibu wagonjwa 885 wakiwa na dalili za ugonjwa huo ,na dadi inazidi kuongezeka karibia kesi mpya 60 kila wiki zinatokea.
Hepatitis E inaambukizwa kutoka kwa mtu na mtu na mara nyingine kwa njia ya matumizi
ya maji na vyakula au kinyesi cha watu walio ambukizwa na virusi hivyo.Taarifa zina
sema kuwa matokeo ya hatari ya magonjwa ya mlipuko ni kubwa kwasababu ya ukosefu wa
upatikanaji wa maji safi .
Kwa sasa ni wafanyakazi 600 wa Shirika la madaktari wa kutoa misaada wa kibinadamu
wako wanafanya kazi ya kubaini kesi mpya za ugonjwa huo na kuwatibu, halikadhali
kuboresha usambazaji wa maji safi katika mji wa Am Timan.
Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni kuweka dawa katika kisima maji kikubwa kilicho juu ya mnara katika mji. Usafishaji wa maji ni kipengele msingi cha dharura ili kuzuia kuenea kwa magonjwa yanayo tokana na maji,kama vile hepatatitis E. Pamoja na kutoa huduma za matibabu katika Hospitali ya Am Timan, Shirika la madaktari wamezindua pia kampeni kwa kiwango kikubwa cha kupulizia dawa katika mabwawa 72 yanayo sambaza maji katika mji wa Am Timan, kadhalika wameanzisha mafunzo kwa ajili ya kueleza umuhimu wa kunawa mikono kwa maji na sabuni, lakini maji yaliyo tiwa dawa, kwa njia hiyo ni dharura ya haraka kuingilia kati zaidi katika suala la maji na usafi.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |