2017-02-12 11:14:00

Tuguse na tuache tuguswe na mwili wa Kristo kwa ukombozi wetu



Ni ziara ya pili ya Kardinali Pietro Parolini Katibu Mkuu wa Vatican  huko Lourdes kwaajili ya tukio la siku ya 25 ya Kimataifa ya wagonjwa inayofanyika tarehe 11 Februari ya kila mwaka sanjari na kumbukumbu ya sikukuu ya Bikira Maria wa Lourdes , ambapo baada ya misa ya Takatifu, Kardinali Pietro Parolini alikaa kwa kitambo akisali katika Basilika ya Mtakatifu Pius wa X Jumamosi mchana.
Mwakilishi maalumu wa Baba Mtakatifu , Kardinali Pietro Parolini pia alitoa tafakari wakati wa maadhimisho ya kuabudu ekaristi takatifu na ibada ya mpako wa wagonjwa.Hali kadhalika akitafakari juu ya wito wa Bikira maria ,Ndimi mtuishi wa Bwana , Kardinali Pietro Parolini aliwatia moyo wanao jitolea na madaktari na kuwahimiza  wawe ishara ya furaha ya uwepo wa upendo wa Mungu kwa wote wanaoteseka.


Kardinali Pietro Parolini pia alikuwa miongoni mwa mahujai wakati wa maandamano ya utamadunisho wa mishumaa kuelekea katika madhabahu, ambapo alikuwa amesema kwamba udhaifu  haufuti kamwe heshima ya asili ya kila binadamu , maana ya utu wa mwanadamu, na  hiyo ni kitu ambacho hakuna mtu awezaye kufuta au kubisha na hilo.
Wakati wa Ibada ya misa Takatifu Katibu mkuu wa Vatican alitoa mahubiri yake  kutoka katika Injili iliyotangazwa katika tukio hilo juu ya Yesu alipoingia katika nyumba ya mwenye dhambi  Simoni Mfarisayo, akakaa kula chakula (Luka 7: 36-50),na mwanamke mdhamb akamuosha miguu yake kwa machozi na kukaushwa kwa nywele zake, na kwamba hiyo ni ishara ya toba.Kwa mujibu wa Kardinali anasema  ni injili inatualika kugusa mwili wa Yesu.

 
Kardinali anasema katika sehemu hii ya injili inatuweka kwenye mitazmo miwili tofauti, kwa kwanza ule wa Simoni Mfarisayo, mtu aliye kuwa ameelimika kiutamaduni na kidini, na mawazo yake ni wazi.Lakini kwa upande wake mgeni aliye mbele siyo nabii halisi na hawezi kumgusa Yesu mwenyewe Kwasababu nabii wa kweli ni yule ambaye anakaa mbali , kwa njia hiyo tunaweza kumuheshimu na kumtumikia.
Na mtazamo wa pili ni wa yule mwenye dhambi bila kuwa na jina , lakini mawazo yake ni wazi kabisa. Yeye mwenyewe anatambua wazi dhambi zake na siyo kujaribu kujihakikisha.Yeye alikuwa kimya na kilio chake, ambacho kinajaribu  kugusa mwili wa Yesu , kwasababu anatambua nabii ni mtu ambaye anaweza kugusa na kuguswa , Kardinali anasema hiyo ni sadaka moja ambayo ilimwezesha kuleta utofauti wa maisha yake na kubadilika.


Hali kadhalika Yesu wakati huo huo aliruhusu aguswe na mtu ambaye alikuwa anadharauliwa , alikuwa mdhaifu mahali pa makutano ,penye heshima na urafiki.Kugusa na kuguswa, anasema kardinali Parolini ina maana ya kuzaliwa upya , kuwa na mwili tofauti , kuwa na roho kwaajili ya upendo , na kwamba kugeuka upya , maana yake hautalinganishwa tena kama siku za nyumba, yaani mdhambi, omba omba, kutafuta madawa ya kulevya,au kujiingiza katika vitendo vibaya.Kugusa mwili wa Kristo na kuacha kuguswa na yeye, Mtakatifu Luka katika Injili anaonesha kwamba sisi sote ni lazima kupitia uzoefu wa nyumba ya Mfarisayo kuliko kukaa katika dhambi.Kipengele hicho kimetoa jina kamili kwa maana ya  kubadilika kwa yule analiye mdhaifu , mwenye mateso na mgonjwa wakati wa upendo , wa uhuru na imani.


Tweet ya Baba Mtakatifu Francisko kwaajili ya wagonjwa

 
Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwenye Tweet katika kilele cha siku ya 25 Kimataia ya wagonjwa tarehe 11 Februari 2017, anawatia moyo na kuwataka watafakari Maria ambaye ni mama wa afya ya wagonjwa,na kwamba ni mdhamini wa huruma ya Mungu kwa kila mwanadamu.

 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican. 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.