2017-02-12 11:35:00

Papa Benedikto XVI bado ni mfano wa umoja wa Kanisa popote duniani


Tarehe 11 Februari 2013 Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita , alitoa tamko la kustaafu utume wa Mtume Petro. Tukio ambalo lilitoa  mshangao mkubwa  sana kwa Kanisa zima , kwa kipindi cha miaka minne tangu kustaafu kwake ,lakini tunazidi kutambua kwa kina zaidi neema kwasababu ya kuona uhusiano wa kindUgu uliopo kati ya Baba MtakAtifu Franciko na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto wa Kumi na sita .Kwa kutafakari zaidi juu ya ushuhuda wa Baba Mtakatifu mstaafu  Benedikto wa Kumi na sita  anao endelea kuutoa kwa  kipindi hiki cha kiroho katika sala ni Padre Federico Lombardi , Rais wa chama Vatican chenye jina la Joseph Tatzinger-Benedikto wa kumi na sita ,alipohojiwa na Mwandishi wa habari wa Radio Vatican. 

Namna alivyoishi wakati wa uongzo wake,ndivyo  anaendelea kuishi miaka hii kwasababu kwani  ni sawa sawa  na maneno yake aliyokuwa ametamka kabla ya kustaafu maana   anaishi kwa sala,kwa mtazamo wa kiroho , katika huduma ya kusindikiza maisha ya Kanisa kwa sala na kwa mshikamano na Baba Mtatifu aliye mrithi katika uwajibikaji,kwa njia hiyo tunaweza kusema unamfanya awe mtulivu wa thati.

Padre Lombardi  anasema amepata kumuona mara nyingi kwa miezi hii na pia  anategemea kuendelea na fursa nyingine tena zaidi baada ya kupewa majukumu ya chama kilicho wekwa jina lake Ratzinger,ambapo itakuwa ni fursa zaidi za kukutana naye mara nyingi. Anasema mara ya mwisho alipokutana naye amemkuta akiwa na utambuzi wa hali ya juu, uwepo wake kiroho, kiakili na hivyo ni anasema inapendeza kukaa naye karibu. Hata hivu nasema kwa hakika kadiri muda unavyopita hata nguvu za kimwili zenyewe zinaendelea kupungua, lakini zile za kiroho ni imara kabisa .

Pamoja na hayo ni mtu ambaye hana magonjwa ya kipekee kwa njia hiyo udhaifu unao onekana ni kwaajili ya miaka inayozidi kuongezeka, lakini yuko kidete na kuweza kutembea kuzunguka ndani ya nyumba,anasisitiza akisema kukaa naye ni kama mzee yote mwenye upunguvu wa nguvu kimwili , lakini mpendelevu wa kukutana naye.

Halikadhalika anasisitiza juu ya kusali kwake kiroho ,ambapo maisha yake, hawali ya yote ni Mungu mi kitovu , imani  kama sababu ya maisha yetu ,hiyo ni kwasababu ya kitabu kilicho andikwa juu ya mahojiano ya Baba Mtakatifu Bebediko kabla ya kustaafu,Padre Lombardi anasema mazungumzo ya mwisho yalikuwa na maana ya ukaribu na kukutana na Mungu, yaani kipindi cha kuishi uzee ni namna ya kujiandaa kukutana na Mungu.
Kwa njia hiyo ni vema kabisa kuwa na Baba Mtakatifu mstaafu akisali kwaajili ua Kanisa na kwaajili ya mrithi wake ambaye ni Baba Mtaktifu Francisko, pamoja hayo hata  Kanisa zima linahisi kwa nguvu uwepo wake wa kusindikizwa na kutiwa moyo wa utulivu wake alio nao.


Aidha Padre Lombardi anaeleza juu ya kuwafahamu  vema Baba Mtakatifu Francisko na Mstaafu Benedikto wa kumi na sita, anatoa ushuhuda wao hasa akikimbuka vema uamuzi wa Baba Mtaktifu mstaafu, kwamaba, tukio hilo lilijitokeza katika hali ya tulivu , na kwa njia hiyo bado linaendelea kuwa uzoefu wa kawaida wa utulivu, kwa wote mnakumbuka vema tukio la uchaguzi , Kardinali Mario ambaye sasa ni Baba Mtakatifu Francisko, alipikutana na Papa mstaafu hakuna aliye kuwa antambua tukio la baadaye, bali Kardinali alikubali alihaidi kutii kwa heshima kwa lolote ambalo linge tukia.

Kwa hiyo Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto wa Kumi na Sita, bado anaendelea kwa utulivu na busara kuishi kwa sala na mshikamano kati ya mrithi wake , nasi ni mashuhuda wa uhusiano huo ambao ni furaha kubwa na mfano wa umoja wa Kanisa popote duniani.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.