2017-02-11 17:00:00

Miaka 49 ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kuzaa matunda tele ya upendo


Ni kuendelea kufanya kazi kwa ushupavu kwa ajili ya amani na maridhiano , mazungumzo kindugu kama wafuasi wa madhehebu mbalimbali. Ni maneno ya Askofu mkuu  Angelo Becciu aliyewakilisha Katibu wa Vatican kwenye maandimisho ya miaka 49 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio Mjini Roma.
Misa ya sherehe hizo iliadhimishwa katika Basilika ya Mtakatifu Yohane Laterano Ijumaa 10 Februari 2017, wakiwemo wanafunzi , wafanyakazi, wazee , watu wasio kuwa na makazi, wakimbizi , wahamiaji , watu wakujitolea , marafiki na wahudumu wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio  Mkuu wa Shirika Marco Impagliazzo pamoja na mwanzilishi Andrea Riccardi


Uwepo hai wa ubunifu wa Kanisa la Roma , kwasababu hatua kwa hatua Jumuiya ya Mtakatifu Egidio imeenea katika makanisa mengi ya ulimwengu, na kupanua kazi mbalimbali , na siyo tu kijiografia , lakini pia katika mgawanyiko wa kazi na mipango mingi.Miradi iliyopangwa haikupotea kwasababu anasema askofu Mkuu , kwa maongozi ya roho mtakatifu mmeongeza ukarimu ambao ukawasaidiwa kufungua njia zaidi mpya na kupanua upeo wenu kwa makanisa mengine.


Akitafakari juu ya masomo ya liturjia , Askofu Beciu anakumbuka mwanzo wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ilivyo jikita kwa watu wenye hali ya kubaguliwa na kutelekezwa. Anasema walia waongozwa na somo kubwa kutoka  kitabu cha mwanzo , mwanaume na mwanamke ni viumbe katika mikono yake Mungu ,wao hubeba sura na mfano wa Mungu, na kwa njia hiyo ni hadi ya binadamu. Aidha anabainisha kwamba mtazamo wa Muumba siyo ubaguzi , hautenganishi katika makundi ya watoto wake: wao ni viumbe wake wapendwa , ambao yeye yuko tayari kujitoa sadaka kwanjia ya mwanae mpendwa, kwasababu anawapenda kama mtoto wake.  Mbele ya binadamu mke , Mungu anatuonesha mashangao na kulipuka kwa kwa kilio cha furaha .Kulingana na somo  hilo Askofu Mkuu Becciu anasema ni kuonesha kwamba kila mtu ni thamani kwa Bwana.


Askofu Becciu anatoa wito wa kuwa na mtazamo wa Muumba kwa kumtazama binadamu yeyote wanaye kutana nao kama mwili mmoja na mfupa mmoja kwani binadamu yeyote anahitaji uangailizi , na upendo wa Mungu ,kila mmoja aweze kumpokea mwingine kama zawadi kwa maana huo ndiyo mkamilishano.Anaelezea shughuli mbalimbali za Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kwa watoto, watu pweke , masikini, kama wito wa Baba Mtakatifu Francisko juu ya utume wa kwenda a kandoni kufanya umisionari katika pande zote za dunia , na hasa sehemu zenye machafuko vurugu, mahali ambapo watu hawatambuliwi haki zao msingi. Kitendo cha kwenda sehemu hizo kinarudisha uwepo wa Mungu katikati na kurudisha utu wa mtu katika maisha ya jamii na maisha ya Kanisa.

 

Akitafakari juu ya Injili ya Mtakatifu Marko 7, 24-30, kuhusu mwanamke aliye kwenda kuomba msaada kwa Yesu mtoto wake apone, Askofu anasema anajisikia kutoa pendekezo la mfano wa mwanamke hasa anayetoka katika nchi ya Syria, na kufananisha na mwanake huyo anayeombea huruma kwaajili ya binti yake.Hiyo ni kwasababu ,mwanamke wa Syria anawakilishwa wanawake wengi wanaoomba msaada wa watoto wao. Wapo wanawake wengi  duniani wanao pata mateso kwaajili ya vita vurugu na ghasia . Mwanamke aliomba msaada wa Yesu na alipofika nyumbani mtoto alikuwa amepona. Kwa njia hiyo ni kama jumuiya ya Mtakatifu Egidio , kwa msaada wa Mungu wameweze kuchangia kupunguza mateso ya mama wengi wanao teseka duniani
Mwisho askofu Becciu anazama Kanisa la Mtakatifu Yohane Lateran ambalo anasema ni Mama Mkuu wa makanisa yote duniani.Kwa njia hiyo Jumuiya ya Mtakatifu Egido imenzaishwa katika kanisa la Roma , na bado inaendelea kuwa muhimu wa uhalisia wa huduma katika Kanisa. Kwa njia hiyo ni lazima kupenda mji na kushirikiana ili mji huo uweze kuwa mzuri na wenye ukarimu.


Uhusiano wa askofu mkuu wa Roma ambaye na baba Mtaktifu francisko, unapaswa kuendelea kwa tabia hiyo si kwaaajili ya mji huu peke yake bali ni upendo katika pande zote za dunia . Na zaidi uzalendo wenu wa Roma uzidi kuwa na ushirikiano mkubwa na Baba Mtakatifu Francisko ambaye anazidi kupanua moyo wake na mikono yake na kuwafikia sehemu ambazo hawezi kufika yeye binafsi kimwili.
Kwa kufanya hivyo italeta maana ya kule mtu awe kitovu na kumfanaya kiala mmoja aliye pemebezoni ajisikie  kuwa kiini cha maisha yake mapya.Ni kwa njia hiyo tunaweza kuleta mabadailiko ya dunia kijiografia na mbegu ya Injili onaweza kuzaa matunda tele ya amani.


Alimazia Askofu Mkuu Becciu kwa kuwashauri warudie wito wa Baba Mtakatifu Francisko alio utoa tarehe 15 Juni 2014 kwaajili yao ya kwamba endeleeni mbele katika njia hii : sala , masikini na amani.Kwa kutembea katika njia hiyo msaidie kuongeza na kukuza huruma katika mioyo ya jamii , ikiwa ni mapinduzi ya kweli ya amani,ile huruma na upole , unao jengan a kukuza urafiki badala ya mizuka ya uadui na utofauti.

Sr Amgela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.