2017-02-10 16:30:00

Gazeti la Civilta' Cattolica kujikita katika uinjilishaji



Wakati Baba Mtakatifu alipokutana na wafanyakazi wa Gazeti la Civilta Catolica , linalo ongozwa na Shirika la Wajesuiti Alhamis 9 Februari 2017, Mkuu wa Shirika la Wajesuiti Padre Arturo Sosa Abascal alitoa salam kwa niaba ya  wote walio kuwapo katika tukio la kuadhimisha  kutangazwa makala ya 4000 tangu kuanza kwake.  Akimshukuru Baba Mtakatifu Francisko uwepo wake karibu katika Jumuiya ya kazi ya Gazeti la Civilta Cattolica, kutokana kuadhimisha miaka zaid ya mia moja katikati ya shughuli za kutoa makala kwaajili ya huduma ya Kanisa na kwa namna ya pekee katika habari za Baba Mtakatifu.


Anasema kwamba ki ukweli katika tukio hili maalumu ambalo Gazeti la Civilta Cattolica , limefikia makala 4000, ina maana kubwa kwani ni zaidi ya miaka 166 katika kujikita kutoa habari njema, masomo mengi yanayohusu historia,siasa , jamii  na utamaduni katika mwanga wake kwa uamninifu na kuwajibika.
Na hiyo inahusu historia ambayo binadamu kwa uzoefu wake anazidi kijikita katika mabadiliko makubwa ya haraka katika nyanja zote za maisha yake, ambapo tunaweza kusema kwamba sisi tuna ufahamu ya kwamba tumeingia katika zama za maarifa baada ya mapinduzi ya viwanda.

Katika muongo huu mawasiliano ya kimataifa yana jukumu muhimu , na kufungua uwezekano  wa maneno ya Injili na utamadunisho wake kusambaa duniani kote.Kwa njia hiyo Gazeti la Civilta Cattolica linapatana nfasi mpya kwa kina kuwa na ufahamu wa changamoto na mapendekezo ya uinjilishaji kwa hatua hii mpya ya mawasiliano ya kimataifa, na kutafuta njia zote mbili za kuunganisha wafanyakazi kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu ambapo inaweza kuzidisha lugha ili kuwawezesha wasomaji . Na pia kwa kutumia akili ya teknolojia mpya zilizoundwa kwaajili ufanisi zaidi wa mawasiliano.

 
Hali kadhali Mkuu wa Shirika la wajesuiti anasema kwa ujumla hatuna nia nyingine zaidi ya tulizo nazo na hasa  sura ya Kristo aliye toa maisha kwaajili yutu msalabani ili wote wanaoishi wapate kuwa maisha tele.Lakini pia tunatambua ya kwamba kwa neema yote yawezekana.Jambo muhimu kwetu sisi ni kuweka matumaini yetu kwake na kuendelea katika uwepo wake kwa maisha yetu na katika maisha ya dunia, na nyumba yetu.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.