Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa maneno ya utangulizi wa hotuba ya Kardinali Montenegro na maaskofu wote waliopo, washauri wa Kitaifa , wakurugenzi wa ofisi za majimbo na wahudumu wote kufika katika tukio la adhimisho la miaka 25 ya siku ya Dunia ya wagonjwa, na miaka 20 ya ofisi ya Taifa katika utume wa afya.Maneno ya utangulizi wa Baba Mtakatifu Francisko alipokutana na wawakilishhi wote wa huduma ya afya ya Italia,katika mkutano ulio andaliwa na Kamati ya huduma na Afya ya Baraza la Maaskofu Katoliki Italia , tarehe 10 Februari 2017 katika ukumbi wa Paulo wa VI mjini Vatican.
Anawashukuru akisema ni hatua muhimu zilizofanywa katika shughuli zote kwaajili ya kuuguza wagonjwa kwa ukarimu wa watu wengi, walio pokea wito wa Yesu katika kuwatembelea wagonjwa kama mfano wake. (Mt 25,36).Hii ni miaka ambayo imeonekana madiliko makubwa , katika utafiti wa kisayansi ulio endelea mbele, na sisi tunatambua tunu msingi na matokeo ya tiba, ambayo wakati mwingine ni inashinda na kutibu magionjwa sugua .Baba Mtakatifu anawatakia heri ya kwamba shughuli hiyo iwe ni kuhakiki wagonjwa wanapewa daima kipaumbele , pamoja na kuathirka kwao, wanaweza kupata unafuu.
Tumsifu Bwana kwa ajili ya wataalamu wengi wa afya , kwasababu ya sayansi yao na maarifa wanatenda kazi kama utume, wahudumu wa maisha na kushiriki upendo wa Mungu Muumbaji,mikono yao kila siku inagusa mateso ya mwili wa Kristo, na hii ni heshima kubwa na jukumu kubwa Baba Mtakatifu anasema. Kadhalika tunashukuru uwepo wa watu wengi wa kujitolea aabao kwa ukarimu wao na umahiri, wanafanya kazi kupunguza na kuonesha ubinadamu wao , kwani wakati mwingine ni kipindi kirefu na kigumu , chenye kujaa upweke , kama wazee, masikini na wahitaji.
Pamoja na taa zinazowaka, ni pamoja na baadhi ya vivuli ambavyo ni tishio linalozidi kuongezeka katika uzoefu wa ndugu zetu wagonjwa.Baba Mtakatifu anasema ya kwamba, kwa upande utamaduni chakavu unao endelea kujionesha katika jamii ya sasa ni katika sekta ya afya. Iwapo mgonjwa hawi kiini cha kufikiriwa kwa hadhi yake, husabaisha mitazamo ambayo hubashiria maafa juu ya wengine.Hii ni mbaya sana , Baba Mtakatifu analalamika na kuongeza kwamba ni muhimu kuwa macho na hasa kwa wagonjwa, wazee wagonja na vilevile walio na magonjwa sugu , ambapo wanapaswa kutazamwa kwa makini halikadhalika wenye kuathirika na magonjwa ya akili.
Mitindo ya vituo vingine vinavyoleta ubaguzi , badala ya kukuza raslimali zilizopo
zinashiria kuzalisha ubaguzi wa binadamu.Kuongeza rasilimali maana yake ni kufanya
matumizi kwa njia ya kimaadili na mshikamano na siyo kuwakumu na kuwabagua walio
wadhaifu.
Baba Mtakatatifu anasema , nafasi ya kwanza inayotakiwa kulindwa ni utu, yaani ulinzi
wa mtu tangu kutungwa kwa mimba mpaka pumzi yake ya mwisho.Siyo fedha tu kuongoza
sera za kisiasa kufanya maamuzi ya utawala ,ni wito wa kulinda haki na afya kwenye
Katiba ya Italia ,na wala siyo uchaguzi wa wale wanao endesha maeneo ya huduma ya
afya.
Ongezeko la umasikini wa afya miongoni mwa makundi ya masikini zaidi ya watu , umetokana zaidi na ugumu wa upatikanaji wa huduma ya matibabu kwani haubagui mtu yoyote tofauti na hivyo ni kuzidisha juhudi za wote kwa sababu ni ya haki kwa masikini na wanao ishi katika mazingira magumu kulindwa. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anatoa uzoefu wa huduma iliyo karibu na wanao teseka na kusema, historia ya Kanisa ya Italia inatambua nyumba nyingi za wasamaria wema, ambapo wote wanao teseka wanapokea mafuta na faraja ,wanapata mvinyo na matumaini.Baba Mtakatifu anaendelea kusema ,yeye anafiri kwa namna ya pekee ya taasisi nyingi za afya katoliki,kwa namna hiyo nawapongeza kwa wema wao na kuwatia moyo waendelee na ndoto ya upendo wa wanaanzilishi wao.
Kwa mantiki hiyo Baba Mtakatifu anatoa wito ya kwamba waendelee kuwa mstari wa mbele bila kukata tamaa kutoa huduma ya upendo mbele ya hali hiyo inayo endelea kuwa ngumu kwa kuoenesha ishara ya huruma ya Mungu kwa masikini ambao kwa matumaini na imani wanazidi kubisha hodi katika nyumba zenu.Anakumbuka ujumbe wa Mtakatifu Yohan Paulo wa Pili akisema , kati ya malengo ambayo Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili alianzisha Siku ya Wagonjwa Duniani , pamoja na kukuza utamaduni wa maisha pia kuna kuhusisha majimbo, jumuiya za kikristo , familia za watawa ni juu ya umuhimu wa utume wa afya (13 Mei 1992).
Wagonjwa wengi wako mahospitalini , lakini pia wengi wako majumbani, ni pweke.Ni matumaini kwamba , wanatembelewa mara kwa mara ili wasijisikie kubaguliwa na jumuiya ,wanaweza kuwa na uzoefu wa ukaribu kwa kila mmoja wanayekutana nao ya kwamba ni uwepo wa Kristo anaye pita katikati ya wagonjwa ambao ni masikini wa kiroho na mwili. Tabia hiyo ya kubagua kwa bahati mbaya inazidi kuongezeka,Baba Mtakatifu analalamika na zaidi ni wagonjwa na masiki na wagonjwa wa afya ,na ukosefu wa kuwaangalia kiroho, wao wanahitaji Mungu na waweza kutoa maisha yao na kupata urafiki na baraka , vile vile, neno la Mungu na kupokea sakramenti na kuwasindikiza katika maadhimisho ya pendekezo la mchakato wa ukuaji na kukomaa katika imani.Anamalizia akisema, kwa neema ya Mungu na kwa Maombezi ya Bikira Maria wagonjwa wanaweza kuwa na nguvu katika udhaifu wao.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |