Ninawakaribisha na kuwashuruni kwa maneno yenu mliyotoa.Ni maneo ya Baba Mtakatifu
Fancisko wakati wa kutoa hotuba yake kwa wawakilishi wa Kamati ya kupinga kashfa,
akisema , watangulizi wake wa kwanza Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili na Benedikto wa
kumi na sita walikuwa wamekwisha kutana na wawakilishi wa kikundi chenu, ambao kuna
uhusiano wa muda mrefu wa Vatican tangu kipindi cha Mtaguso wa Pili wa Vatican .
Ninatambua na kufurahi ya kwamba mahusiano hayo yameendelea kwa kina ,na kwamba kama
mlivyoeleza juu ya mkutano wenu, ni ushuhuda muhimu na zaidi ya hayo ni majukumu
, kwa nguvu ushirikiano unaleta uponyaji na kueneza mahusiano,kwa namna hiyo ninawashukuru
na pia Mungu naye anafurahi kuona urafiki wa kweli wa kindugu kati ya wayahudi na
wakristo. Ni kama isemavyo zaburi ya 113,1.3 ni jinsi gani ndugu wawili kuishi pamoja
kwa manai maana pale Mungu anatoa baraka na maisha daima.
Kama utamaduni wa makutano na maridhiano huzaa maisha, na kuleta matumaini, kinyume
na kuwa na utamaduni wa chuki upanda kifo na mavuno yake ni kukata tamaa. Baba Mtakatifu
anatoa mfano kwamba mwaka jana amekwenda katika makambi ya mateso na ukatili huko
Uholanzi (Birkenau). Hakuna maneno na mawazo ya kutosha kueleza tukio la namna hii
ya ukatili dhidi ya wayahudi , bali ni sala kwa Mungu aweze kutoa huruma kwaajili
ya majanga ya namna hiyo na yasirudiwe mara nyingine tena.Kwa njia hiyo tutaendelea
kusaidiana moja baada ya mwingine , kama wito wa Mtakatifu Yohane Paulo wa pili alivyosema
naye kwamba, "katika kufanya kumbukumbu ya utekelezaji wa majukumu, ni muhimu katika
machakato wa kujenga maisha endelevu juu ya uovu wa ukatili huo isirudiwe tena .(Barua
ya Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili 12 Machi 1998).
Baba Mtakatifu anasitikitishwa na kashfa ambazo hadi leo bado zinajotokeza akisema
“kwa bahati mbaya kupambana na kashfa mbaya juu ya wayahudi , tabia hii bado imeenea
na inajitokeza kwa aina tofauti kinyume na kanuni za Kikristo katika maoni ya kila
mwanadamu anavyo stahili.Kwa mjibu wa Katiba unasema " Kanisa Katoliki inawajibu wa
kufanya kila iwezekanavyo na marafiki wote wa kiyahudi kupinga na kupambana na tabia
za ubaguzi na kashfa."
Halikadhalika Baba Mtakatifu Francisko anasema kwamba leo kama ziku zilizopita, mapambano ya kupinga kashfa inawezakana kwa njia ya kuelimisha. Kwa maana hiyo anawashukuru kwa kazi yao ya kuongeza kampeni za kupinga kashfa kwa njia ya elimu na kuendeleza heshima kwa wote na kuwalinda wadhaifu.Kulinda hazina ya maisha ya binadamu tangu kutungwa kwake hadi mwisho wake wa kuishi.Kulinda heshima ni njia bora ya kuzuia aina zozote za vurugu .Mbele ya janga la fujo ghasia na vurugu zilizotapakaa katika dunia , tunahimizwa zaidi katafuta amani bila vurugu, kwaajili ya kukuza yaliyo mema.
Anamalizia akitoa mfano ya kwamba iwapo tunataka kupalilia magugu ya ubaya, ni dharura
ya kupanda yale yaliyo mazuri , kupalilia haki , kuimarisha maelewano, kuunga mkono
ushirikiano na siyo kukata tamaa . Kwa nia hiyo tunaweza kuvuna matunda ya amani .Kwa
hiyo ninawatia moyo nikiwa na matumaini ya kwamba kuweka zana muhimu za kuhamasisha
utamaduni ambao unathamini kila mahali uhuru wa dini, na kulinda watu wake wa kila
dhehebu dhidi ya vurugu na nguvu, pia vyombo vya kuweza kusitisha chuki zisitawale.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |