2017-02-08 16:18:00

Justus Takayama Ukon ni shahidi wa kuigwa kwa Wakristo wa Japan


Kardinali Angelo Amato Rais wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza waumini watakatifu na wenye heri, Jumanne 7 Februari, aliadhimisha ibada ya misa ya kumtangaza mwenye heri Justus Takayama Ukon huko Osaka kwa niaba ya Baba Mtakatifu francisko .
Wakati wa ibada takatifu ya misa alitoa mahubiri kuhusu huyo mwenye heri mpya  Justus akisema , alikuwa ni mwenye shahuku kubwa ya kuinjilisha nchini Japan, ambaye kweli alikuwa ni mpiganaji wa Kristo kwa maneno na matendo yake. 
Justus alizaliwa mwaka 1552 na kifo chake 1615 , alilelewa katika maisha mazuri amabayo baadaye akaweza kukomaa zaidi wakati alipokutana na wamisonari wa kijesuiti, na kukomaa baadaye kwa imani ya Kristo , na akawa mwenye nguvu zaidi hadi kuchukiwa , na kulazima kukimbilia uhamishoni katika nchi nyingine.Hiyo ilimfanya kupoteza fursa zake na kuishi maisha ya umasikini, lakini hakusikitishwa na hilo, bali kwa upole hadi furaha ya kuwa mwaminifu kwa ahadi ya ubatizo.


Kabla ya kufukuzwa Nagasaki , alihukumiwa kwenda uhamishoni nchini Ufilippini akiwa na wakristo wengine mia tatu na walifika Manila baada ya safari ngumu na ndefu baharini iliyodumu siku 43. Alikuwa tayari ameshakuwa mdhaifu na mgonjwa na hivyo Justus akafa ufilippini baada ya siku 44 tu za kufika . Alikuwa na miaka 63, lakini ushuhuda wake wa imani kubwa kwa kristo ulikuwa ni wa hali ya juu katika wakati mgumu wa migogoro na mateso.Kardinali Amato baada ya kukumbuka maisha yake aliongeza pia  JUstus aliishi kikristo bila kufikiria kwamba Injili ilikuwa tofauti na utamaduni wa Japan , bali kuwa karibu na wamisionari wa kijesuit alijikita zaidi katika kutangaza Injili na sura ya maisha ya Yesu aliyejitoa maisha kwa ajili ya ukombozi wa watu  kutoka utumwa wa dhambi na mauti.

 

Hiyo ni kwasababu katika siku zake za mwisho Justus aliendelea kukazia mazoezi ya kiroho , kwa sala, sakramenti , na kujitenga katika  ritiriti za kiroho na wamisionari. Hivi vilikuwa kama nyenzo madhubuti za kumsaidia katika kupokea kifo na kutoa maisha yake kwaajili ya uongofu wa Japan, akisali na kuwasamehe watesi wake.Alitaja jina la Yesu na kutoa roho yake kwa Bwana kama alivyo fanya shahidi Stefano.Mwisho Kardinali Amato anatafakari konesha juu ya urithi wa mwenye heri Justus alio waachia  wakristo wa Japan ya kwamba,  yeye aliishi kwa imani , aliishi akithamini mila na desturi za utamaduni wao.Kwa tabia yake ya dhati ya kiinjili aliyokuwa ameirithi .Yeye alikuwa ametambua ujumbe wa kiini cha Yesu ambao ulikuwa ni Upendo .Kwa njia hiyo ya huruma kwa watu walio kuwa anawaongoza , alikuwa akisaidia masikini , alikuwa wakiwapatia mahitaji muhimu . Alianzisha chama cha ndugu wa huruma, Aliwatembela wagonjwa , alitoa sadaka na alisaidia kuwazika wafu wasio kuwa na ndugu .

 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.