2017-02-07 16:22:00

Papa anasema utofauti wa imani katika maadili bado ni changamoto


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 6 Februari 2017 alikutana na waakilishi wa Kiekumene wa Makanisa ya Kienjili ya Ujeruman, katika hotuba yaka alimshukuru Askofu wa Kanda Bedford-Strohm kwa maneno ya hotuba yake na pia kushukuru uwepo wa Kardinali Marx Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Ujeruman akiwa mojawapo wa wshiriki wa Mkutano huo, na kusema ni tunda la ushirikano na mshikamano wa muda mrefu katika mahusiano ya kiekumene ambayo yanakomaa kwa miaka.Anawatakia mema ya kuendelea mbele katika njia hii iliyobarikiwa katika umoja wa kidugu , kwa kufuata kwa ujasiri na maamuzi kuelekea muungano  kamilifu kwasbabu ya kwamba tunao ubatizo mmoja na tunapaswa kutembea pamoja bila kuchoka.

Lina maana sana tukio la Maadhimisho ya miaka 500 ya Mageuzi ya Kiluteri Duniani na Wakatoliki wanachukua fursa hii kuadhimisha kwa pamoja matukio ya kihistoria yaliyotoke ambapo tunaweza kuweka kwa pamoja Yesu we kitovu cha mahusiano. Akikumbuka juu ya mahusiano , anasema tafakari kuhusu Mungu , Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa XVI alipokutana  na wawakilishi wa Makanisa yaa Kiinjili huko Ujerumani 23 Septemba 2011 lisema ni namna gani tunaweza kutambua jinsi tulivyo na Mungu mwenye huruma” akiwa anaelezea juu mwanzilishi wa mageuzi hayo Martin Luther Ambaye kwa shahuku kubwa alikuwa akiwahamasisha juu ya njia ya kufuata kuelekea Kristo .

Baba Mtakatifu anasema na hiyo ndiyo  njia tunawajibika kuwa nayo yaani  moyoni wa kina na dhati baada ya kuanza upya njia ya umoja na maridhiano. Katika kuadhimisha mwaka huo tunalazimia kupiga hatua mbele , tukitazama mambo yaliyopita bila hasira , bali kwa matashi ya Kristo katika umoja naye ili kuwatangazia watu wote habari mpya ya msingi wa Yesu , na huruma yake isiyo na kikomo. Kama vile walivyofanya mageuzi ambayo yalileta utengano kati ya wakristo, ni  jambo ambalo halikuwa jema, kwasababu watu hawakujisikia  kuwa ndugu tena   katika imani bali maadui kati yao na kushindana kwa muda mrefu ambapo vikazuka vizingiti ma mapambano na kuingiliwa na mafao katika sera za kisiasa na utawala hata bila ya kujiuliza matatizo ya kufanya ghasi hizo dhidi ya ndugu.

Leo hii Baba Mtakatifu anasema, tunamshukuru Mungu kwaajli ya muungano mara kwani jitihada zao za kuwa pamoja kwa unyenyenekevu na uwazi kukabiliana na kupindi kizito na kichungu kuisha na kuweza kushirikishana ishara muhimu za kitubio na maridhiano ambayo leo hii uponya majeraha ya kumbukumbu zilizopita  katika ushuhuda wa Kristo. Wakatoliki na Waluteri wa Ujerumani mnaweza kujibu  hilo kwa njia ya sala na mwaliko kwa watu wote katika nchi ili kuendelea na kujitakasa kwa Mungu wakati wa kufanya kumbukumbu.Anawashukuru kwa umoja wa kiroho ambao kwa miaka hii mingi umekuwapo katika njia ya kiekumeni na ambayo leo hii watu wote wasali kwa pamoja kuondokana na kushindwa muungano huo kwa kuchuchumilia zaidi umoja katika mantiki ya mageuzi ya maendeleo endelevu.

Hiyo ni kwa sababu wote tumebatizwa ubatizo mmoja unaotufanya tuwe ndugu kwa njia ya roho mtakatifu , na kutambua utofauti wetu ambao umekuwa sasa mapatano , tukisifia hata zawadi za kila mmoja wetu alizo nazo za kiroho na katika mageuzi yaliyokwisha patikana. Tofauti kuhusu imani katika maadili , hadi sasa bado upo na kuendelea kuwa changamoto katika kuelekea umoja, ambao unakabili ndugu.Uchungu mwingi umewapata hasa wana ndoa walio tofauti na dhehebu zao, lakini kwa muda huu na  mwafaka inabidi kujitahidi kusali kwa nguvu zote il kuweza kubakibilina na vizingiti hivyo ambavyo bado vipo, na kujikita hasa katika mafunzo ya kiteolojia , katika mshikamano wetu na  kwaajiliya huduma kwa wale wote wenye kuteseka,na kwaajili ya kulinda mazingira. Dharura kubwa ya Yesu kwa wanafunzi wake ni umoja (Yh 17,21) tunaalikwa binadamu wote katika kipindi hiki ambacho kuna uzoefu wa mageuzi mapya  na katika mengi yanayo jitokeza, na hiyo inawewezekana ikawa wajibu wetu mkubwa.Kwa matumaini ya mkutano wenu tunaweza kukua katika muungano kati yetu , na tuombe roho Mtakatifu aweze kufanya umoja kuwa mpya. 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.