2017-02-07 16:02:00

Mungu ametupatia damu yake na kutukabidhi ardhi ili tuitunze


Binadamu amefanywa kwa mfano wa Mungu na akepewa mke wa kupenda .Kwa njia hiyo binadamu kapewa zawadi tatu ambazo Mungu amezawadia binadamu wakati wa kazi yake ya uumbaji .Ni maneno ya Baba  Mtakatifu Franciscko wakati wa kutakari katika misa ya asubuhi tarehe 7 Februari 2017 katika Kikanisa cha Mtakatifu Martha kilichoko mjini Vatican. "Mtu ni nini ee Mungu hata umfikirie, ulimvika utukufu wako…". Baba Mtakatifu anahubiri kutokana na somo la kwanza  kutoka kitabu cha  mwanzo na sehemu ya kiitikio kutoka zaburi 8 kuonesha ukuu wa maneno ya upendo wa Mungu  kwaajili ya viumbe wake, na kuongeza ,Mungu alitupatia damu yake kama watoto kwasababu tunafanana naye.

Mungu ametujalia  zawadi tatu, hawali ya yote sisi ni damu yake tukafanywa watoto wake ,kwasababu ametuumba  kwa sura na mfano wake. Anatoa mfano ya kwamba Mtu anapo jifungua mtoto hawezi kuwa kinyume,maana mtoto yuko mbele yake ki ukweli,na mtoto huyo anafanana na baba yake au wakati mwingine hapana lakini ni mtoto wake na mzuri,lakini ikitokea kidogo ni mbaya ,hawezi kumkana kusema  mbaya bali atasema  mzuri tu maana ni mtoto wake  na amemsubiri kwaajili yake … Hali kadhalika ndiyo maana Yesu alitufundisha kama Baba yake ambaye anasubiri watoto wake. Alitupatia huo utambulisho wa mtoto awe mke au mme sisi sote ni watoto wa Mungu.

Dunia imekabidhiwa kwa binadamu aitunze Baba Mtakatifu anasema , kwaajili ya kazi tu nasiyo  kuharibu , na hiyo diyo zawadi ya pili ya Mungu anayotujalia katika uumbaji ni kazi kwasababu Mungu alitupatia ardhi kuitawala kama isemavyo somo katika kitabu cha Mwanzo  na hiyo ni urithi ambao Mungu alimpatia binadamu kwasababu Mungu hataki utumwa  wa watoto wake bali  wawe Bwana , yaani mfalme akiwa na kazi.Kama yeye alivyofanya kazi wakati wa kuumba , naye pia anatukabidhi sisi tuendeleze kazi ya uumbaji. 

Hatupaswa kuharibu , bali kuifanya ikue na kuitunza , Yey alijitoa kwa yote .Baba Mtakatifu anatoa mfano kwamba Mungu hakutupatia fedha , Je fedha hizo nani alizitoa? Anasema hajui bali anasema kwamba mababu walisema ni shetani aliingia katika mifuko, na kwa hiyo tunaweza kufikiria nani alitupatia fedha…. Lakini kwa kutunza kazi ya uumbaji na kuendeleza ni zawadi, na ndiyo maana mwisho Mungu aliumba mke na mme kwa mfano wake aliuumba. Baada ya utawala juu ya uumbaji , ndipo tunapata zawadi ya tatu ambayo inatajwa katika kitabu cha mwanzo nayo ni upendo unao unganisha mke na mme.Mme na mke Mungu aliwaumba , Siyo vema  mwanaume aishi peke yake, na ndiyo maana ampatia mwenza . Baba Mtakatifu anaendelea kusema Mungu upendo alimpatia mwanaume upendo na hiyo ni mazungumzo ya upendo ambayo ndiyo hatua ya kwanza kwa binadamu na mkewe.

Mwisho Baba Mtakatifu anashukuru Bwana kwa ajili ya zawadi hizo tatu tulizo jaliwa ambazo ni utambulisho, ya kazi na upendo ambapo tuombe Mungu aweze kutufanya tutunze huo utambulisho wetu,na kufanya kazi juu ya zawadi tulizopokea na kuendelea na kazi zetu za kila siku, na neema ya kujifunza kila siku kupenda zaidi.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.