Wapo zaidi ya wamisionari 50 na watawa 14 kutoka nchi tofauti za dunia wanao toa
maisha yao katika nchi ya Mongolia, wao ni waaminifu katika wito na kuendeleza uhusiano
wa kina na Mungu kwaajili ya kujitoa zaidi kwa jamii na kwa ndugu. Ni kwa huduma hiyo
imewezesha Kanisa la Mongolia kujiandaa kuandimisha miaka 25 ya umisionari, ambapo
muda si mrefu pia wataweza kufungua parokia tatu.
Padre Prosper Mbumba wa Shirika la Moyo safi wa Bikira Maria kutoka nchi ya Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo DRC akiongea na Shirika la Habari la Fides wakati wa kuadhimisha
sikukuu ya Bwana kutolewa Ekaluni tarehe 2 Februari sanjari na siku ya watawa duniani
kila mwaka anasema, ni fursa kwao kutafakari wakiwa pamoja na Askofu Mkuu Wenceslao
Selga Padilla Balozi wa kitume wa Papa huko Ulaanbaatar.
Halikadhalika miongoni mwa watawa wengi waliokusanyika, Sista Nirmala mtawa wa kiindi
kutoka katika Shirika la Moyo safi wa Bikira Maria anaeleza juu ya uzoefu wake wa
maisha ya kitawa ya kwamba, amefika nchi ya Mongolia miaka zaidi ya 10 na kwamba ni
mtawa kwa miaka 18. Sista huyo anakumbuka ya kwamba mwaka jana 2016 Kanisa la Mongolia
lilifanya sikukuu kubwa kwa mzaliwa wa kwanza kupata daraja la upadre na kwa mwaka
2017 ni jubileo ya miaka 25 ya umisionari wa Kanisa baada ya kuondokana na mfumo
wa utawala wa kikomunisti.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |