Kodi ya maendeleo ya Ulaya imetenga miradi kufanya kazi katika nchi zenye kiwango za juu zaidi cha wahamiaji wanaopitia bahari ya meditranea ili kusimamia utekelezaji wake kwa wahamiaj hao.Ni pendekezo la Katibu mkuu wa Chama cha wafanyakazi (UIL) Carmelo Barabagallo,nchini Italia wakati wa mkutano wa Kimataifa kwa mara ya kwanza huko Lampedusa kisiwani Italia tarehe 1 Februari 2016 wa kauli mbiu “kwaajili ya bahari ya amani na Kazi”
Kati ya washiriki wa mkutano huo walio toa hotuba mjumbe kutoka nchi ya Tunisia wa
tuzo ya amani kwa mwaka 2015 Hassine Abbassi anasema ukosefu wa ajira pia ni chanzo
cha wahamiaji kupita baharini na pia anapinga kile kiitwacho ugaidi unaopangwa , ambapo
anasema ndiyo chanzo kikubwa cha wahamiaji, kwani serikali nyingi zimechagua njia
za ugaidi kwa madhumuni ya kujitajirisha binafsi, hata kwa gharama ya uharibifu wa
nchi nzima.Aidha anasema mapinduzi ya nchi ya Tunisia, yamefanikiwa dhidi ya umasikini
na haki ya kijamii kwa kupata kazi,uhuru na ugawaji sawa wa utajiri.
Na mwakilishi wa kipalestina Husain Fogahaa katika hotuba yake anakumbusha kwamba
ni milioni 6 ya wapalestina wako nchi za ugenini duniani kote na wengi wako katika
makambi ya wakimbizi. Anaongeza, japokuwa walikubali Serikali ya Israel , lakini leo
hii ni zaidi wa vituo vya ukaguzi 400 vinavyozunguka nchi nzima na kuwanyima haki
zao msingi.Anasema “Sisi Wapalestina ni wahamiaji katika nchi yetu." Asilimia 28%ya
watu wasio kuwa na ajira na wengi wanaishi katika hali ya umasikini.
Wahamiaji haramu ni vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 35 , na wengi wao ni wahitimu
wa elimu ya juu, kama wataalumu wa compututa na sayansi , ni wana uchumi lakini wanakabiliwa
na kipeo cha ukosefu wa ajira. Taarifa inaeleza kwamba sababu kubwa ya kiuchumi na
ukosefu wa ajira, ukosefu wa kuhama kwa njia halali, na vyombo vya habari kuchochea
picha zinazo onesha utajiri wa jamii za Ulaya , ni mojawapo ya sababu msingi zinazosababisha
uchaguzi wa wengi kuhama. Hamu ya kusafiri imezidi kuongezeka kwa miaka 25 hivi, na
hasa kwa miaka ya karibuni ni vijana wengi wanao kuja katika nchi ya Italia wakifiria
kupata msaada.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |