2017-02-03 13:14:00

Maaskofu Italia kusaidia miradi 119 kwa nchi zinazoendelea


Zaidi ya euro milioni 18 zimapangwa kufadhili nchi 119 katika dunia , kiwango hiki kimetengwa na Kamati ya Baraza la Maaskofu wa Italia kwaajili ya kutoa huduma kusaidia nchi zinazopiga maendeleo, kwenye  mkutano  uliofanyika hivi karibuni mjini Roma.
Taarifa zinasema ,miongoni mwa  miradi iliyo mikubwa ya kufadhiliwa  ni katika nchi Ghana kwaajili ya ujenzi na kuandaa vifaa vya matibabu   katika kitengo  maalumu kwa wangonjwa wenye matatizo ya viungo kama mishipa  na mifupa ya mwili katika kituo  kiitwacho  Yohane Paulo wa II kwenye Jimbo la Kinongo –Mampong Ghana.Ni kituo muhimu sana kutokana na msongamano mkubwa wa idadi ya watu na wote wana mahitaji kulingana na ajali nyingi barabarani kupitia Jamasi barabara kuu inayounganisha Mkoa wa Ashanti na mikoa ya kanda ya kaskazini ya nchi.


Katika nchi ya Jamhuri ya Kati , fedha hiyo itaweza kujenga kituo cha elimu cha  kisaikolojia na kituo cha huduma ya afya ya wagonjwa wa akili kwenye Jimbo kuu la Bangui , kwa kusaidia watoto ambao wamepata matatizo ya kisaikolojia kutokana na migogoro na ghasia ya nchi.Itakuwa kwa mara ya kwanza ujenzi wa kituo hicho katika nchi .
Katika nchi ya Jamhuri ya kidomokrasia ya Congo,ambayao kwa miaka 10 imefadhiliwa na chama cha Tumaini katika mji wa Goma,mji ambao umekuwa uwanja wa fujo na ghasia na kusababisha vifo vya maelefu ya watu , mradi unao lengo la kuendeleza jukumu la wajane na watoto wao.Kituo hicho kitatoa huduma ya mafunzo ya elimu kama vile kusoma na kuandika, teknolojia ya sayansi na komputa, warsha za kitaalam kama vile (kushona , kupika,ufundi) ili kuboresha hali ya maisha ya familia na upatikanaji wa ujuzi kwa shughuli za kuzalisha kipato.


Na Amerika ya Kusini ni katika nchi ya Guatemala, mgao huo utasaidia mfululizo wa mikutano kati ya viongozi wa wakulima na malezi ya wake zao, ili kubadilishana uzoefu katika kuimarisha sekta za kilimo na usalama wa chakula katika Parokia ya mama yetu wa Guadalupe. Na mwisho miradi miwili itakuwa katika nchi ya Kurdistan na Papua Guinea .Kwa upande wa wa Kurdistan ni kuwasaidia watu waliosongamana na wakazi wanaoishi katika mji wa Erbil na katika wilaya ya Kirkuk katika mji wa Ak Kosh. Na Papua Guinea ni ujenzi wa majengo mapya ili kupanua makazi yao.


Kwa ufafanuzi zaidi wa fedha hizo Shirika la Habari Sir linasema euro  9,000.637, zitasaidia miradi 53 kwa Afrika , euro 2,947.597 miradi Amerika ya Kusini , euro 3.194.573  miradi Barani Asia ; Euro 2.068.780 miradi nchi za Mashariki; euro 721.871; miradi 3 ya Ulaya Mashariki ; euro 350.584 kwa mradi mmoja  huko Bara la Austraria .Kwa jumla ni euro milioni 18.284.042 .

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radi Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.