Serikali ya Uingereza lazima kuongeza mara mbili jitihada zake za kutekeleza mageuzi gerezani ili kuboresha mfumo wa magereza katika kuokoa maisha ya watu, ni ombi la Maaskofu wa Uingereza na Wales katika taarifa yao iliyotolewa mara baada ya Wizara ya Sheria na Haki ya Uingiereza kutoa ripoti juu ya matukio ya wafungwa kujinyonga wenyewe ndani ya magereza.Kwa bahati mbaya ni idadi inayoeleza bayana juu ya maabusu kwa uamuzi wao wenyewe na visa hivi vinazidi kuongezeka.
Kwa mujibu wa ripoti ni kwamba inaonesha kwa mwaka 2016 maabusu 119 wamejinyonga
wenyewe na kesi 34,784 ni ajali za kujidhuru wao wenyewe na vilevile matukio na vurugu
25,049, hizo ni takwimu za kutisha na hazikubaliki, anasema Askofu Moth Arunde na
Brighton wakarugenzi wa makanisa ya wafungwa , wakionesha pia uhaba wa wafanyakazi
na msongamano wa wafungwa ambao ndiyo sababu msingi ya uwepo wa matukio kama hayo
ndani ya magereza.Pamoja hayo wanaonesha kwamba mwaka jana , kumekuwa na maandamano
ya maofisa wa magereza kuhusu afya na usalama kazini , wakati huo wafungwa wengi walionesha
kuwa na matatizo makubwa.
Takwimu za sasa juu ya kujinyonga na vitendo binafsi vya kujiumiza wenyewe ndani ya
magereza , Askofu Month anasema ni vya kushtua , kwani Kila janga la kifo binafsi
ni kuumiza familia yake na wafanyakazi ndani ya magereza wanao jaribu kuzuia vifo
hivyo.Kutifia hatua hiyo ya matukio ndani ya magereza , ni jamabo lisilokubalika na
anaongeza, inabidi kushughulika kwa haraka masuala yanayohusiana na wafanyakazi na
pia msongamano wa wafungwa , na kuhakikisha huduma nzuri na muhimu wafungwa na hata
wenye ugonjwa wa akili vinapatikana.
Skofu Arundel na Brighton wanakumbuka kwamba Mwandishi Dostoyevski , aliandika kwamba
"kiwango cha ustaarabu wa jamii unaweza kuhukumiwa kwa kuingia katika moja ya magereza
yake ".Kwa nja hiyo ni wajibu wa kila mtu ili kupambana na hali hii.Kwa maana hiyo
wito wa Askofu kwa serikali ni kufanya kwa haraka iwezekanavyo ili mageuzi gerezani
yawepo .Kwa upande wa Kanisa la Uingereza na Wales wanasema kwa pamoja na mapadre
wanao hudumia kanisa la magereza na watu wa kujitolea waendelee na juhudi za kusaidia
wafungwa wanaoishi katika mazingira magumu, aidha na kufanya kazi pamoja na taasisi
na watu katika vituo vya kizuizi.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |