Tunaomba wanafunzi warudi mashuleni kwaajili ya kuendelea na mwaka wa masomo wakati
huo wakiendelea na kampeni zao halali.Ni maneno ya Maaskofu wa Baraza la maaskofu
katoliki wa Afrika ya kusini , kwenye ujumbe ulio tiwa saini na Askofu Mkuu William
Salatterry Askofu Mkuu wa Jimbo la Pretoria kwa niaba ya maaskofu wote.
Kwa miezi hii wanafunzi wa Afrika ya kisini wanapinga kuongezeka kwa kiwango cha malipo
ya Chuo Kikuu , na maandamamo hayo yamesababisha baadhi ya matukio mengi ya ajali
kati yao na nguvu za vyombo serikali.
Kadhalika wanafunzi wanatarajiwa maandamamo ya kupinga yaanze bada ya ufunguzi wa
mwaka wa masomo, na kwa njia hiyo Maaskofu wanaomba kwanza wanafunzi waweze kufikiria
namna ya kuweza kufikia malengo ya kampeni zao bila kuvuruga mipango ya kitaaluma
na bila ya kusababisha ghasia.Aidha maaskofu wanatoa ahadi ya kutoa msaada wao kwani
wabasema, elimu inapaswa ipatikane kwa watu wote kwa kutegemea usawa na uwepo wa mazungumzo
ya upatanisho kati ya sehemu zote mbili, kwamba wanatambua zaidi juhudi na mafanikio
yaliyo patikana nchini Afrika ya Kusini katika sekta ya elimu lakini pia wanaomba
uwepo wa mwongozo wa uamuzi thabiti kutatua mgogoro huo.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |