2017-02-01 15:52:00

Maaskofu wa Cada kulaani kitendo cha mashumbulizi ya Msikiti


Canada katika Kanisa la Notre-Dame –de Foy Quebec ilifanyika misa ya kuwaombea waathirika 6 waliopoteza maisha yao katika mashambulizi ya msikiti mkuu wa Kiislam. Misa hiyo iliadhimishwa na Kardinali Gérald Cyprien Lacroix Askofu Mkuu wa Jimbo hilo."Machozi ya uchungu yamewapata jumuiya ya Quebec lakini inabidi kufanya uamuzi wa kutokukubali maovu na chuki".Ni maneno ya Kardinali Gérald Cyprien Lacroix, wakati wa ibada ya misa jioni ya Jumanne 31 Januari 2017.

Shirika la habari la Sir limemkariri akisema kwamba anawashukuru wote kwa ushuhuda na mshikamano kwa kipindi cha uchungu na kuwaombea ndugu wote waathirika wa Jumuiya ya kiisalam walioshambauliwa na kwamba, Mungu aweze kuwasaidia wapate nguvu mpya kuendelea mbele katika ule upendo ambao ni muhimu katika kuishi kwenye nchi ya amani na ushirikiano, na kusema “matumaini yetu yameweka  majaribu kwa njia hiyo tuinue sala zetu kwa Mungu wa umoja na muumba,ni Baba yetu wa kila huruma.”

Kabla ya ibada ya misa alitoa neno mmoja kati ya  waanzilishi wa kituo cha utamaduni wa kiislam Boufeldja Benabdallah kwa machozi alitaja majina yote sita ya waathirika akikimbuka  kila mmoja na kazi yake aliyokuwa akifanya.Halikadhalika anasema “ asante kunikaribisha kwa maana ninyi ni marafiki” na pia "katika dini yetu, unapotaka kumweleza  mtu mwingine juu ya upendo ulio nao inabidi kumwambia moja kwa moja, na hivyo hata mimi ninasema kwamba ninawapenda”

Alitoa historia ya kkufika kwake mjini  Quebec kwa miaka 48 ilioyopita, mji ambao ulimfungulia mikono yake, kama vile ulivyo tenda kwa hao waliopoteza maisha yao."Tulifika  katika mji huu mzuri na wa kustaajabisha ni  mahali ambapo tulichagua kuishi na kuwakuza watoto na familia zetu, nyinyi ni watu wema ,na tumejifunza kutoka kwenu mambo mengi na hasa namna ya kuishi na wengine ,msamaha na heshimu ya watu wengine, kwa hayo yote tunatoa sifa na utambuzi huo".

Halikadhalika anasema watajibidisha kuwaeleza watoto wa waathirika ya kwamba siyo mji wa Quebec walio uwa baba zao, bali ni ubinadamu ulio kosea na kufanya kile ambacho hakutakiwa kufanya, kwani tunawakikishia kutambua vema  wema wa moyo wa binadamu,kwa hiyo hatutaweza kuruhusu hasira na chuki viweze kuingia katika mioyo ya watoto.
Na wakati wa sala kabla ya matoleo ya sadaka  , aliyesoma maombi hayo ni Khadija Said wa jumuia ya kiislam, na Dekano wa kianglikana wa Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Christian Schreiner wakiombea waathrika na waamini wa madhehebu yote na kwamba, kwa jina la Mungu wa huruma isitokee tena aina yoyote ya nguvu na migogoro kwa watoto na vijana ambao ndiyo matumaini ya dunia mpya, kwaaajili ya Kanisa ,kwaajili ya diplomasia ya kimataifa katika shughuli za kuleta amani na kusitisha migogoro ya kivita na misuko suko.


Na ujumbe kutoka katika Baraza la Maaskofu wa Canada kuhusiana na tukio hilo; Maaskofu wa Canada wameshutumu kitendo kibaya cha mashambulizi ya kituo cha utamaduni na sala cha Kiislam huko Quebec katika ujumbe wao ulio tiwa saini na Rais wa Baraza la maaskofu wa Canada Douglas Crosby askofu wa Jimbo la Halimilton.Katika maandishi  ya Gazeti la Sir , maaskofu wanaonesha mgutuko wao na kulaani vitendo hivyo vya vurugu  ambavyo vimeacha mauti ya watu.Halikadhali katika maadishi hayo wanasema huo ni ukiukwaji  na ukosefu wa heshima katika katika maeneo matakatifu na pia kwa  maisha ya binadamu , kwasababu aliye shambuliwa  anayo haki na uhuru kama mwanachama wa dini zote kukusanyika na kuomba kwa kina  kulingana na imani zao.Hayo ni mashambulizi yaliyosababisha majeraha ya amani,utulivu wa nchi na jamii yake katika kunajisi maeneo ya sala na ibada. 

Pia Askofu Lionel Gendron,  wa Saint Jean-Longueuil (Quebec)  anasema janga hili la kikatili limetokea katika jamii yetu iliyokuwa inasemekana kulindwa dhidi ya hatari hiyo na kwamba  ni miezi sasa jamii nyingi miongoni mwao zikiwa ni parokia ambazo zimejikita kukaribisha kwa furaha wakimbizi wengi, na hasa kutoka nchi ya Syiria na wengi  wao ni waislam. Waislam wengi walifikiri wamefika mahali pa utulivu na sasa wanarudiwa ofu kwa upya.

 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.