2017-02-01 15:38:00

Maaskofu Marekani watoa ombi la utetezi wa heshima ya binadamu


Wito wa Maakofu wa Marekani kwa ajili ya kutetea heshima ya utu wa binadamu umetolewa kutokana na kukosoa hatua iliyotolewa na Rais mpyaTrump kutokupokea wakimbizi ndani ya nchi yake.Tendo hilo limekuwa tayari ni joto binafsi la maaskofu wa Kamati ya Baraza la Maaskofu wa Marekani anayeshughulia idara ya wakimbizi Askofu Joe Steve Vasquez wa Jimbo la Austin aliye waeleza Viongozi wa Baraza la maaskofu wa Marekani wakati wa kikao chao.
Taarifa ya saini ya rais na makamu wake , Kardinali Daniel N.na di Nardo Askofu Mkuu wa Galveston –Houston, Askofu Mkuu José Horacio Gómez wa Jimbo kuu la Los Angeles ,wanatoa wito kwa waamini wote katoliki wawe na sauti moja , kwaajili ya kutetea heshima ya utu wa  binadamu.Kwa upande wa maaskofu siyo kwamba wanaingilia moja kwa moja  maandamano ya kisiasa ya umma,bali ni kukumbuka Injili isemayo kwamba kumpokea mgeni ni miongoni mwa utume wa maisha ya mkristo.

Akitoa mfano kutoka katika kipengele cha Mtaguso wa Pili wa Vatican,hasa katika tamko la “nyakati zetu”(notra aetate) maaskofu wanabainisha msingi wa nguvu ya upendo na haki isiyo kuwa na mwisho ambayo ndiyo uhusiano uliopo kati ya Wakristo na Waislam. Wakisikistizia  kuwa Kanisa, halitakosa kamwe kutetea  ndugu wote wa madhehebu yanayo kabiliwa na mateso na unyanyasaji mikononi mwa watesi wao.
Kwa maana hii, wanakumbusha  kwamba wale ambao hukimbia  kutoka katika serikali ya Kiislam na katika vikosi vingine vyenye msimamo mkali wanajitoa sadaka ya kila kitu hata kile chenye thamani katika miliki yao kwa jina la mani na uhuru." Hawa ni watu binafsi na familia ambao wanatafuta usalama kwa watoto wao.

Kwa njia hiyo maaskofu wanatoa wito  juu ya mapokezi. Bila shaka ni lazima kuwa macho kuhusu hatari  ya uwezekano wa kuingiliwa na vikundi vya kigaidi katika taifa, lakini wanapaswa kuwakaribisha na kuwaona kama wao ni washiriki wa kupambana na maovu yote.Wanasema kwamaba  Kwani mahali ambapo hakuna mapokezi ya watu,ni bayana vitendo vya  ubaguzi na kutelekezwa kutokea, na hivyo maaskofu wanasema wao watakuwa sauti kwa niaba yao.

 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.