2017-01-31 14:45:00

Wanawake na masikini ni waathirika wa mabadiliko ya tabianchi


Ni wanawake,masikini zaidi wanaowathirika na mabadiliko ya tabia , sisi ni wahudumu na siyo watawala wa uumbaji, ambapo tunalazimika kimaadili kutunza na kulinda: ameyasema maneno hayo katika Shirika la Habari la Fides Kardinali Gracias, askofu Mkuu wa Bombay na Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu barani Asia,(Fabc), kabla ya kumaIizika mkutano wao ulio andaliwa hivi karibuni na Baraza hili kuhusu mabadiliko ya Hali hewa, ya kwamba ni makundi ya wanawake na masikini waathirika zaidi.Katika mkutano huo wawakilishi 45 kutoka nchi ya Bangladesh, Nepal, na India, ambao ni wahudumu kutoka katika  ofisi za Taasisi, Sekretarieti , na kamati zinazo jihusisha na mabadiliko ya tabia nchi.


Mkutano huo ulitaka kujikita juu ya kutafakari za sera za mabadiliko ya tabia nchi , na juu ya makundi ya waathirika wa hali hiyo. Mkutano umetoa fursa ya kushirikisha na kufanya majadiliano juu ya mipango iliyopo, katika kufafanua zaidi namna ya kuweka katika matendo mema kukabiliana na hali hiyo ya tabia nchi, kwa kufanya utafiti wenye uwezekano mpya wa maendeleo endelevu katika kujibu kwa pamoja wakiwa na mpango mmoja wa matendo ndani ya kanda zao.Akiongea na Fides, Kardinali Gracias anakumbuka kwamba binadamu wote tunazo fursa za kukabiliana na madiliko ya tabia nchi kwasabu ni matatizo ya ulimwengu mzima, unaakabiliwa na maafa makubwa zaidi ya mazingira,kijamii, kiuchumi kisiasa , na kwamba ni moja ya changamoto ya kibinadamu ambayo kila siku anakabiliana nayo.

Naye Askofu Allwyn D’Silva Katibu mtendaji wa Ofisi ya maendeleo ya Binadamu wa Fabc alisema .“Nchi zilizo endelea zimekuwa  za kwanza kuhusikakatika uharibifu kwa kupasha joto sayari hii.Wakati huo huo nchi zinazo piga maendeleo ndiyo zinalipa matokeo mabaya  ya maendelea kiuchumi na kidharura kama nchi zetu barani Asia na kusini,tunatoa  gesi ya ukaa ya kwasababu ya kukidhi dharura yao ya maendeleo. Halikadhalika,ni vema ya kwamba nchi zote  zikatambua ya kwamba  hali ya hewa ni kwa manufaa ya wote,na wote tunapaswa kuwajibika.Binadamu wote wanaalikwa kutambua vema mahitaji ya mabadiliko na hasa namna ya kuishi kuzalisha,au kutumia , wapate kupambana na upashaji joto wa sayari hii hata kujua sababu kwamba ni binadamu mwenyewe anayehusika na uharibifu wa mazingira, hayo yalisemwa na Deepika Singh mratibu wa ofisi  inayojishughulikia madiliko ya tabia nchi ya Baraza la maaskofu wa Asia.


Anaongeza Askofu Jacob Mar Barnabas rais wa Baraza kwaajili ya wanawake katika Baraza la maaskofu wa ndia akisema  kazi msingi ya Kanisa la Asia ni kujibu wito wa kila mbatizwa , na kila binadamu kuongoka kwa dhati, na kuachilia  mbali hali matumizi ya  kuzidi kiasi,ili  kuchagua maisha yanayo stahili, katika kufanya upya utamaduni wa kuheshimu kazi ya uumbaji, kujikita kwa undani zaidi katika matumaini na furaha.Jumuiya Katoliki kwa mtazamo huo ukiongozwa na mafundisho jamii ya Kanisa , wanapaswa kukukuza mikakati ya mipango kama vile ya teknolojia ya kijani ,uzalishaji endelevu wa kilimo, na kuwajibika katika matumizi,namna ya kutenganisha vitu na kivisindika kwa upya, vilevile kuhamasisha haki kati ya vizazi.

Ili kukabiliana na madiliko ya hali ya hewa , inahitaji mshikamano, na mwelekezo msingi wa manufaa ya wote, ambao unaweza kuongezwa kwa njia ya mchakato wa elimu na tafakari katika kanda ; hayo pia anasema Katibu mtendaji wa Ofisi ya Baraza la maaskofu kwa upande wa walei na familia, kwa njia hiyo Maaskofu wa Asia wataendelea na huduma hiyo katika sekta hiyo kwa ngazi za majadiliano tafakari na matendo.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.