Tume ya Kipapa kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto wameipongeza Kanisa Katoliki Zambia kwa kuwalinda watoto na watu wazima wanao ishi katika mazingira magumu.Katibu Mkuu wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya ulinzi wa watoto Monsinyo Robert Oliver anasema,Kanisa la Zambia linapaswa kupongezwa kwa kuzungumza kwa moyo wote na kuchukua hatua katika kushughulikia suala la unyanyasaji wa watoto.
"Nilipokutana na Askofu Mkuu , aliongea kwa nguvu juu ya mahitaji na ya kuhakikisha
kwamba kila mtoto ni salama na anakua katika mazingira ya Amani na upendo.Yapo mambo
yanayo tokea hapa nchini Zambia ya kusisismua na kupengezwa" .Anasema Minsinyo Olver
.
Halikadhali anatoa wito kwa jamii ya kutojihusisha na unyanyasaji wa kijinsia,pia
dhidi ya kufanya ngono kwa mtoto yoyote.
Anasema "Unyanyasaji wa kijinsia kwa mtu ni mbaya. Hatupaswi kuficha wahalifu hawa;
haijalishi kama ni mtu mwenye mamlaka katika Taasisi, mapadre katoliki, mjomba au
Baba.Tunapaswa wote kwa pamoja kupinga viendo hivi.Kwa njia hiyo ni kazi yetu kupitia
mashirika yote ya dini katoliki, vyama vya kiraia na wengine".
Monsignor Oliver aliyasema hayo alipokuwa Zambia kama mjumbe kwenye warsha ya siku
moja huko mjini Lusaka, Jumatatu,23 Januari 2017. Kauli mbiu ya warsha ilikuwa juu
ya "haja ya kutekeleza Sera katoliki juu ya ulinzi wa Watoto na wanaoishi katika
mazingira hatarishi katika jamii" kama kama wito wa Baba Mtakatifu Francisko , kwani
amewataka Kanisa kufanya maamuzi ya kuwalinda watoto na vijana wa dunia nzima.
Kutoka Amecea Blog
All the contents on this site are copyrighted ©. |