Uwepo wenu ni sababu ya furaha yangu kuwapokea wakati mmeunganika katika Mkutano Mkuu wa Mwaka kwa kutafakari juu ya Imani kwenye kujikabidhi,na Hotuba yake aliyoitoa Rais wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Taasisi za kitume pia salam kwa wote nikiwaonesha kuitambua kazi yenu katika huduma ya maisha ya kitawa kwa Kanisa.
Ni maneno ya utangulizi wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko alipokutana na washiriki
wa Mkutano wa Mwaka kwa mashirika ya maisha ya Kitawa na vyama vya kitume Jumamosi
28 januari 2017 mjini Vatican. Anasema kauli mbiu mliyochagua ni muhimu , ambapo tunaweza
kusema kwa nyakati hizi uaminifu ni changamoto ya majaribu, kutokana na takwimu mlizo
onesha.Baba Mtakatifu anatoa mfano kwamba chanagamoto hiyo inafananishwa na damu zisizosimama,
ambazo udhoofisha maisha ya kitawa na Kanisa yenyewe.Kitendo cha wengi kuacha utawa,
kinaleta wasiwasi mkubwa.Ni kweli kwamba wengine wanaacha kutokana na sababu za msingi
, kwasababu wametambua nafsini mwao mara baada ya safari yao ya kiroho ua kwamba
hawana wito, lakini licha ya hayo wapo wengine ambao wanakosa uaminifu, anaongeza
na kusema hayo yanajitokeza mara tu baada ya kufunga nadhiri za milele ,Je ni kitu
gani kimesababisha ? Ni swali Baba Mtakatifu anauliza.
Kama vile mlivyo onesha ya kwamba zipo sababu zinazosababisha ukosefu wa uaminifu,
kwa njia hiyo mabadiliko ya mihongo na siyo tu mabadiliko ya mihongo , bali jinsi
ya kuweza kukabiliana na utata na kuchukua majukumu thabiti ya kudumu.
Sababu ya kwanza inayofanya kutokutunza uaminifu ni mazingira ya kijamii na utamaduni
tunamoishi.Tunaishi katika utamaduni ulio gawanyika vipende vipande ,kwani kitendo
cha kutaka kutunisha mfuko, unamfanya mtu aishi kwa mitindo . Huo ni utamaduni unaofanya
mtu kuishi akitegemea milango mingine ya pembeni inayofungua uwezekano mwingine.
Kitendo cha kutegemea milango hiyo inaongeza matumizi na kusahahulisha uzuri wa wa
maisha rahisi na ya kina na kusabaisha utupu wa kuishi.
Baba Mataktifu anaelezza kwamba,imejitokeza sababu za vitendo vya mahusihano kulingana
na jinsi kila kitu ni kuhumu katika suala binafsi ,na mara nyingi ni tofauti na maadili
ya Injili. Tunaishi katika jamii ambapo sheria za kiuchumi huchua nafasi ya kwanza
zaidi ya maadili , Watunga sheria hulazimisha kwa manufaa yao mwenyewe , wakikandamizu
thamani ya maadili ya maisha.Na hiyo ni jamii ambayo udikteta wa fedha na faida zake
umwondolea yule ambaye hana uwezo , kwa mantiki hiyo ni wazi kwamba mtu lazima kwanza
ache kuhubiriwa ,na ajibidishe baadaye kuhubiri.
Katika sababu ya Utamaduni jamii, tunapaswa pia kuongeza sababu nyingine. Mojawapo
ni ulimwengu wa vijana , huo ni ulimwengu tata Baba Mtakatatifu anasema , wakati huo
pia umejaa changamoto. Lakini hapakosekani hata vijana wakarimu, wenye kuwa na mshikamano
na wanao jibidisha katika ngazi ya mambo ya kidini na kijamii.Ni vijana wanaotafuta
ukweli wa kiroho, vijana wenye njaa ya jambo flani tofauti ili wapate kuipeleka duniani.Baba
Mtakatifu anasisitiza kwamba wapo ndiyo vijana wakarimu na siyo wachache. Pamoja na
hayo, wapo miongoni mwa vijana waathirika katika mantiki ya kiulimwengu , ambao wanatafuta
sifa , kwa njia zozote, au fedha rahisi na anasa.
Mantiki hii inawaada vijana wengi, na hivyo hughuli yetu kubwa , siyo tofauti ya
kukaa karibu nao kwa kutoa ushuhuda wa Injili ya furaha itokayo kwa Kristo.Ni utamaduni
unao paswa kuwahabarishwa iwapo hatutaki vijana wasitafunwe na ulimwengu huu.
Sababu ya tatu ni ile inayotoka ndani ya maisha yenyewe ya utawa ,kwani mbele ya ukaribu
wa utakatifu Baba Mtakatifu anasema hapakosi hali ya kutokuonesha ushuhuda , ambayo
hufanya uaminifu kuwa mgumu. Kati ya hali hizo ni sababu hizo za ndani ya jumuiya
ni pamoja ukawaida, uchovu,madaraka ya usimamizi wa nyumba, mgawanyiko wa ndani, kutafuta
ukuu,shirika kutawaliwa na mitindo ya kiulimwengu, au namna ya kutawala kibavu wakati
mwingine husababisha mazoea ya kufanya hali ya maisha yaende hivyo.
Baba Mtakatifu Francisko anatumia maneno ya Mtakatifu Paulo ya kwamba iwapo maisha
ya utawa yanapaswa kubaki katika utume wake , yanapaswa kubaki katika msimamo wake
, na kuendelea kuwa katika shule ya uaminifu kwa walio karibu na mbali.(Ef 2,17),Inapaswa
kutunza upya wake na habari mpya ya kiini cha Kristo kwa njia ya roho na nguvu ya
kitume , kuonesha uzuri wa kumfuasa Yesu na kuangaza kwa matumaini na furaha.
Moja ya eneo lionapaswa kutilia umakini wa kutunza katika kutunza maisha ya kindungu
ndani ya jumuia.Ni lazima kulishwa kwa sala , kusoma Neno, kushiriki kikamilifu katika
sakramenti ya ekaristi , ya maridhiano na mazungumzo ya kindugu , na kuwa na mawasiliano
ya dhati kati ya wanajumuiya wake, aidha kusahihishana kindugu, kuanzia huruma kuelekea
kwa ndugu aliye kosa , na kwa kushirikishana majukumu.
Yote hayo yafanyike kwa furaha na ushuhuda wa maisha rahisi , hasa kujitoa kwa masikini
wanaoishi pembezoni.Vilevile kufanywa upya katika maisha ya kidugu ndani ya jumuia
, inategema sana na utume wa miito , usema njoo na uone ( Jh 1,39) na kuishi kwa pamoja
kindugu wawe vijana au wazee .Na hiyo ni kwasababu kama kijana hapati mahitaji muhimu
katika maisha ya kitawa ndani ya jumuiya atakwenda nje kutafuta .( Soma Ujumbe wa
maisha ya Jumuiya ya watawa wa Tarehe 2 Februari 1994, 32).
Wito ni kama vile imani hiyo ni tunu ambayo tunaichukua kwenye mtungi wa mfinyanzi (2 Kor 4,7) kwa namna hiyo tunapaswa kuitunza kama watunzavyo vito vya thamani, ili baadaye isije ibiwa hiyo tunu hiyo na wala kupoteza uziri wake baada ya kupita muda .
Wajibu huo hawali ya yote ni kwa kila mtu ambaye ameitwa kumfuata Yesu Kristo kwa
karibu kwa imani , matumaini na Upendo. Hivyo Baba Mtakatifu ana waalika kujihimarisha
kila siku katika sala na kuweka nguvu kwenye mafunzo ya kiteolojia na mafunzo ya
kiroho, ambayo inapinga na kuzuia mitindo ya utamaduni wa kisasa ili kuweza kutembea
kidete katika imani.
Kwa misingi hiyo ni wazi kwamba upo uwezekano wa kufuata mashauri ya kiinjili na kufanana
na mawazo ya Kristo(Fil 2,5). Wito ni zawadi ambayo tumeipokea kutoka kwa Bwana,inayojikita
upendo wake kwetu sisi alivyo tupenda (Mk10,21) na kutuita tumfuate katika maisha
ya kitawa,wakati huo unawajibisha kila mto aliyepoka zawadi hiyo.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |