2017-01-29 10:41:00

Kamada mkuu Hoffmann von Rumerstein kuongoza Jeshi la Malta


Baraza kuu la Shirika la Kijeshi la Malta lililokutanika mjini Roma tarehe 28 Januari 2017 limeridhia uamuzi wa Fra’ Matthew Festing kung’atuka kutoka madarakani kadiri ya kipengele namba 16 cha Katiba ya Malta. Baba Mtakatifu Francisko ametaarifiwa rasmi na kwamba, taarifa hii pia itatumwa kwa wakuu wa nchi 106 ambao wana uhusiano wa kidiplomasia na Shirika la kijeshi la Malta. Kadiri ya kipengele namba 17 cha Katiba ya Shirika la Kijeshi la Malta, Kamanda mkuu Hoffmann von Rumerstein ameteuliwa kuwa ni kiongozi mkuu wa mpito hadi pale uchaguzi mkuu utakapofanyika tena. Bwana Albrecht Boesalager ataendelea na cheo chake ndani ya Jeshi hili.

Baraza kuu la Jeshi la Malta limetumia nafasi hii kumpongeza Fra’ Matthew Festing kwa sadaka na majitoleo yake kwa muda wa miaka tisa, kama Kiongozi mkuu wa Malta. Katika barua ambayo Baba Mtakatifu Francisko amemwandikia Fra’ Matthew Festing, kwa mara nyingine tena amependa kukazia uhusiano wa dhati kati ya Vatican na Jeshi la Malta na kwamba, Kamanda mkuu Hoffmann von Rumerstein anashika madaraka katika kipindi hiki cha mpitoa, ambacho kimekuwa tete kidogo. Ni matumaini ya baba Mtakatifu kwamba, huu utakuwa ni muda wa kupyaisha tena maisha ya kiroho kwa wanachama wake wa kudumu pamoja na kuonesha ushirikiano wa dhati na mwakilishi maalum atakeyeteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko mwenyewe.

Taarifa inaonesha kwamba, Jeshi la Malta linapenda kumpongeza na kumshukuru Baba Mtakatifu Francisko pamoja na Kardinali Pietro Parolin kwa kuguswa na maisha na utume wa Jeshi hili katika kushuhudia imani na kutoa huduma makini kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamiichangamoto ambayo itawasaidia kukuza na kudumkisha maisha na utume wao duniani!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.