2017-01-27 16:21:00

Maangamizi makuu dhidi ya Wayahudi Ulaya yasitokee tena


Katika siku ya  kukumbuka maangamizi makuu  dhidi ya Wayahudi Barani Ulaya  Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi tarehe 27 Januari 2017 amekutana na wawakilishi wa kiyahudi  wa Barani ulaya mjini Vatican kwa mazungumzo, na alikuwepo Padre Norbert Hofmann Katibu wa Baraza la kipapa la Mahusiano ya kidini na Wayahudi.ambaye baada ya mkutano alihojiwa na mwandishi wa habari wa Radio vatican kuhusiana na mkutano. Padre Hofmann anasema mkutano huo uliwakilishwa na wajumbe watano wa Mkutano wa Wayahudi Ulaya ambao wanawakilisha wayahudi milioni mbili Barani Ulaya , na mkutano huo ulikwenda vizuri ambao kulikuwa wa kawaida na wenye mawazo mazuri.Baba Mtakatifu Francisko ameanza na mazungumzo akigusia juu ya siku kumbukumbu hiyo ya maangamizi ya Wayahudi Ulaya lakini pia akasema ni siku inayo tuhusu watu wote kutokana na waathirika wengi walio poteza maisha yao na vitendo vya maangamizi ya namna hi visitokee tena.

Na kwa upande wa mwakilishi mmojawapo  Moshe Kantor amesema juu ya umuhimu wa maadili na thamani ya wakristo na wayahudi waliyo nayo kwani dunia hii tunamoishi mandeleo yamekuwapo, japokuwa bado kuna changamoto ya kuanguka kwa maadili, na hivyo ni wajibu wa kuhamasisha thamani hizo zilizopo kati ya wakristo na wayahudi.Na siyo tu bali pia umuhimu wa mafundisho ndani ya familia. Kwa upande huo, Baba Mtakatifu amemuunga mkono kutokana na kuanza kusimulia historia yake ya maisha yake ambayo imefanya mkutano wao kuonesha matunda ya mazungmzo kati ya wayahudi na wakristo. Baba Mtakatifu ametoa mfano kwamba katika familia yake walikuwa wakipokelewa wayahudi, na katika utoto wake ameishi katika hali hiyo ambapo wayahudu wengi walikuwa wakenda nyumbani kwake, na yeye amekuwa rafiki wa wayahudi.Na mwisho wa Mkutano wao wote waliufurahia , na hivyo padre Hofmann anasema ni sisi sasa tunapswa kuhimarisha ushirikiano huo na wayahudi.

Maangamizi makuu dhidi ya Wayahudi wa Ulaya yalikuwa mauaji ya Wayahudi milioni 5-6 wa Ulaya wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia kati ya mwaka 1940 na 1945. Mauaji haya yalipangwa na kutekelezwa na serikali ya Ujerumani chini ya Adolf Hitler kwa msaada wa serikali za nchi zilizofungamana na Ujerumani au zilizokuwa chini ya jeshi la Ujerumani.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.