Waliweka Mkataba wa makubaliano wa Hosptali ya watoto Bambin Gesu ,huko Bangui
nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati , kwa nia ya kuwaandaa madaktari wapya . Maombi
hayo ni mpango thabiti ulio pendekezwa na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa ziara
yake ya kichungaji Novemba 2015.
Hayo ni maneno ya Daktari Mariella Enoch Rais wa Hospitali ya watoto Bambin Gesu
Mjini Roma ambaye amepata kusema alipohojiana na mwandishi wa habari wa Radio Vatican,
kuhusiana na hospitali hiyo kwamba, alikwenda kutembelea Bangui miezi mitatu iliyopita
na kukuta miradi ya Baba Mtakatifu aliyoitamani inaendelea bega kwa bega na kwamba
hali ya wakimbizi kwa sasa ni kama inakaribia kuisha.Anasema watu wanaendelea kurudi
katika majumba yao kwa msaada waliopewa.
Na katika ziara hiyo Daktari Enoc anasema walipata kusahini Mradi wa kwanza wa Hospitali
ulio kuwa unatarajiwa , napia kutia sahini kwa mradi mwingine na Waziri wa Elimu
kwa suala la Chuo Kikuu cha mafunzo ya madaktari na pia kwa Waziri wa Afya kwaajili
ya kitengo cha maabara ya viungo ambayo inatakiwa iwe pamoja na hospitali ya watoto
huko Bangui.Kwa upande wa Daktari Enoc anasema hicho kilikuwa ni kitendo rasmi ambacho
kwasasa tunawajibika kufanya kazi pamoja na Serikali kwaajili ya nchi.Aidha anasema
kwamba pamoja na hayo kuna Mashirika mawili yasiyo ya kiserikali ndani ya kituo cha
Hospitali ya watoto ,ambapo kwa wakati huu ni lazima kujaribu kutafuta namna ya kushirikiana
kwa pamoja , wamezoea kufanya kazi wao peke yao bilashaka wataweka juhudi zao kuweza
kushirikiana kwa pamoja.
Na matumani yetu kwamba sasa wataanza mapema kukarabati Hospitali ambapo mwezi Septemba pia wataanza kazi halisi ya Chuo Kikuu cha mafunzo ya madakatari na hasa watoto, kazi hiyo anasema , watafanya wao kuwafundisha madakatari zaidi wa watoto kutokana kwamba baadhi ya madaktari waliopo hakuna anayeweza kufundisha,kwa njia hiyo daktari anasema itakuwa mafunzo kwa ujumla , watakao ifanya wao, lakini wanayo furaha kuifanya.
Daktari Enoc anasema jinsi ilivyo anza mradi huo kwamba, wazo lilitokana mara baada ya Ziara ya Baba Mtakatifu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, yeye Mwenyewe aliwaoomba wakuu wa Hosptali hiyo aweze kuisiamia, mara baada ya kuitembelea na kuona hali halisi ilvyokuwa ngumu .Baada ya kurudi Roma alimwita Daktari Mariella kwa mkutano na kumuona ashughulikie mradi huo kati ya miradi ya hosptali.
Jambo la kufurahisha anasema Daktari ni kwamba wao wanafanya kazi kwa ushirikiano
na chi na siyo kufanya kazi kwaajili ya nchi. Kwa njia hiyo na kweli juhudi kubwa
ya kushirikishana na mamlaka ya nchi ambao ndiyo wanao wajibu wa huu ili kuifanya
nchi iweze kukua ndani yake.Paomja na hayo Dkarari anasema inahitaji juhudi kubwa
ya kufanya hospitali mpya na uendeshaji wake iwapo kuna utashi , pia anafikiri Daktari
Enoc ya kwamba ni sawa na mawazo ya Baba Mtakatifu asemayo kwamba ni kusaidia ukuaji
kwa ujumla wa nchi.Licha ya miradi hiyo kuna hata mradi mradi mwingine wa kilimo ulio
kabidhiwa katika Shirika la Wakarmeli huko Bangui ya kwamba , ni mradi muhimu kwasababu
baada ya kuwakabidhi nyumba , kinachofuata ni kuanza kuwapa kazi na wakati huo huo
afya, na hii Daktari anasema ni kama vile Baba Mtakatifu aliweza kuchukua kwa ujumla
nchi yote.Lakini kwa dhati naweza kusema , mabadiliko yanaonekana kwa miezi miwili
tu.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |