2017-01-25 16:32:00

Monsinyo Viganò: toeni habari zinazofumbata kweli na haki!


Wakati Baba Mtakatifu Francisko anatoa wito kwa kutoa habari njema , haimanishi tu maudhui yaliyomo katika habari hiyo, bali ni kuwaangalia  kwa macho wale wanao toa habari hiyo.Baba Mtakatifu hataki vyombo vya habari kuwaeleza watu simulizi za kama vile za watoto kitoto.Hayo yalisemwa na Monsinyo Dario Edoardo Viganò, Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Mawasiliano mjini Vatican, wakati wa  kuwasilisha Ujumbe wa 51 wa Siku ya Upashanaji Habari Duniani uliotolewa na Baba Mtakatifu Francisko, 24 Januari 2017.Mkutano huo ulifanyika na waandishi wa Habari katika ofisi za habari mjini Vatican.

Akigusia pia juu ya habari zinazotolewa juu ya janga la kuanguka kwa Hotel moja  nchini Italia ambayo imesababisha operesheni inayoendelea ili kuokoa wathirika kuwa ngumu, Monsinyo Viganò anasema kuna njia ya kutoa habari  ya ukaribu, njia ya kuwasiliana ambayo inaruhusu hata Taasisi kuanza mara moja shughuli, ni kutoa habari zinazofaa kwa upande huo  kwa wakazi wa Italia , ambapo habari hizo zinakuwa ni kielelezo katika kuanza mshikamano Hiyo ndiyo maana ya kuwasilisha kweli ukaribu, kwa sababuni habari unayosaidia kuamka na kuanza kutoa msaada . Zitolewe habari za kuonesha uwezo wa watu kujieleza ukarimu wao kwa tukio kama hilo la kutisha.

Pamoja na hayo yote Monsinyo Vigano anabainisha , wakati mwingine ni kunyume kabisa na itikadi za kisasa, kwasababu maono ya itikadi ni ambayo haina ukaribu, kwani wakati mwingine yupo lakini hatambui mwenzake  aliye karibu kinacho msibu  japokuwa  anafikiria  anajua kila kitu hata bila ya kuona. Kwa njia hiyo , Monsinyo Vigano anasema ni kama kuweka sumu katika visima, akiwa na maana ya  kwamba ni kutoa taarifa usio kuwa na uhakika au ukaribu ni sawa na kuweka sumu katika jamii , akaongeza sisi tunajua kwamba shetani na watoto wa ubaya, wanazaa mitafaruko tu.

Monsinyo Vigano alikumbuka mkutano kati ya Rais wa Israel Shimon Peres na wa Palestina Abu Mazen , uliofanyika mjini Vatican tarehe 8 Juni 2014. Katika hafla  hiyo anasema wanasiasa hao wawili , walisali kwa pamoja na kupanda mzeituni.Hakika katika mkutano huo , si kwamba matatatizo yao yalitatuliwa , lakini jambo hili lilkuwa ni muhumu na lenye nguvu, kwasababu hiyo kila mmoja alikaa karibu na mwenzake, huo ndiyo ukaribu.
Halikadhalika  Monsinyo Vigano akielezea juu ya uzushi wa taarifa za uongo zinazosambazwa , anasema kwamba daima ,uzushi wa habari za uwongo una nguvu za wakati huo , kwasababu ni habari zinazosambaratika kwa haraka , lakini zinadumu kwa muda mfupi.

Kwa mtazamo huo , Vigano anasema siyo kwamba Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake, hana wasiwasi juu ya habari za uzushi na uongo, bali napendelea na kuwashukuru wale wanao kuwa na mtazamo wa kukosoa, japokuwa katika kukosoa wanapaswa kukosoa kwa upendo na ukweli. Kukosolewa kwa viongozi au makundi ni muhimu kutokana  na kujisahihisha ili waweze kuongoza na kufanya vizuri zaidi.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.