Mwakilishi wa Papa katika Baraza la kipapa la maendeleo endelevu ya Binadamu Askofu Giampiero Dal Toso alikwenda kutembelea Aleppo akiwa na Kardinali Mario Zenari ,Balozi wa Kitume huko Syiria na Mons Thomas Habib Kuanzia tarehe 18 -23 Januari 2017.Hiyo ilikuwa ni ziara ya kwanza maalumu kwa wawakilishi wa Vatican inapolekea kumalika kwa vita ya Aleppo.Wawakilishi hao walipata kukutana na jumuiya za kikristo na wachungaji wao, ambao walimshukuru Baba Mtakatifu Francisko , kwa juhudi zake za kuhamasisha misaada ya Syiria. Pamoja na hayo waliwatembelea Taasisi Katoliki na pia makambi ya wakimbizi.
Kwa namna ya pekee walifanya uzinduzi wa chombo cha kibinadamu kinachoendeshwa na
Caritas ya Aleppo katika mtaa wa Hanno.Wakati wa ziara hiyo pia walifanya sala na
maombi ya kiekumeni kwaajili ya tukio la wiki ya maombi ya umoja wa wakristo inayoendelea
, na walijionea hali halisi ya uharibifu wa vituo vya afya katoliki , ambapo kwa
mwanga zaidi vinaweza kukarabitiwa na vikaweza kufanya kazi.
Licha ya hayo walifanya mkutano pia na wawakilishi wa dini ya kiislam na wote walisistiza
jukumu la kuelimisha dini , amani na maridhiano.Wakati wa ziara hiyo pia viongozi
wa nchi na madhehebu walitoa pongezi kubwa kwa Baba Mtakatifu Francisko ,kumteua
Kardinali mpya kutoka katika nchi yao na kusema hiyo ina maana ya kutambua ukaribu
zaidi wa papa na watu wa Syria.
Katika mikutano na Tasisi za kutoa huduma katoliki waliona umuhimu wa msaada unaotolewa
kwa manufaa ya watu wa Syiria. Kwa msaada wa Kanisa zima la Ulimwengu na juhudi kutoka
katika jumuiya za kimataifa , na msaada huo unaweza kuimarisha na kujenga wakati
ujao na kukidhi mahitaji mbele ya ongezeko la watu .Miongoni mwa dharura hizo , kuna
haja na kuangalia hasa vitu vinavyohusiana na mahitaji muhimu kama chakula mavazi
, elimu , afya na makazi .
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
All the contents on this site are copyrighted ©. |