Kufanya mapenzi ya Mungu haimanishi usibishane au kumkasirikia Bwana , la muhimu
uwe mkweli na iswe mnafiki na mwishowe ukamwambie “tazama mimi hapa”,ni maneno ambayo
yamejitokeza katika mahubiri ya Baba Mtakatifu Jumanne 24 Januari 2017 wakati wa Misa
Takatifu katika Kikanisa cha Mtakatifu Martha Mjini Vatican .
Kiini cha mahubiri ya baba Mtakatifu Francisko ni kutoka katika barua ya Wahebrania
iliyosomwa ya siku “wakati Kristo alipokuja duniani, wewe hukupendezwa na dhabihu
na sadaka ya kuteketezwa na kuondoa dhambi. Tazama mimi ninakuja kufanya mapenzi yako”.
Hili neno la Yesu alisema Baba Mtakatifu , linafunga historia ya “tazama mimi hapa
“maana yake ni historia ya wokovu .Baada ya Adamu aliyekuwa mafichoni kwasababubu
ya hofu ya Bwana , Mungu alianza kumwita , na akasikia sauti ya mmojawapo walio kuwa
wamejificha ikiitikia “mimi hapa “maana yake “niko tayari”. Tazama mimi ni kuitikia
kwa Ibrahimu, Musa, Eliya, Isaya , Yeremia hadi kufikia mimi hapa ya Maria ambayo
ilikuwa ya mwisho wakati wa kuchukua mimba Yesu. Ni historia ya tazama mimi hapa
lakini siyo ya moja kwa moja kwasababu Mungu anazungumza na wale anao karibisha.
Baba Mtakatifu anaendelea kuelezea kwamba, Bwana anaongea na wale anaowakaribisha
ili waweze kutembea katika mwelekeo huo “tazama mimi hapa. Yeye ana uvumilivu mkubwa
, kwani tunaposoma katika kitabu ya Ayubu, maneno na tafakari ya Ayubu ambaye hakuelewa
na wala kujua majibu , ambayo Bwana alimwambia na kumkosoa, Lakini mwishowe ile ndiyo
ya Ayubu kwa Bwana na kusema wewe una haki,kwani mimi nilikujua tu kwa kusikia tetesi,
na sasa macho yangu yanakuona wewe .Ni kusema ndiyo wakati ukiwa na utashi , kwani
maisha ya kikristo ndiyo hayo ya kusema tazama mimi hapa” kuendelea kufanya mapenzi
yako Bwana. Ni vizuri kuendelea kusoma neno katoka katika Biblia Takatifu na kujaribu
kutafuta majibu ya watu wanao itikia wito kwa Bwana, na kwa kupata jibu hilo ni jambo
zuri sana , Baba Mtakatifu alisema na kuongeza, mimi hapa niko tayari kufanyua mapenzi
yako.
Baba Mtakatifu Francisko anatoa maswali mengi akitumia mifano kutoka katika Biblia
Takatifu akisema:Je Ninakwenda kujificha kama Adamu ili ni sijibu? Au wakati Bwana
akiita , badala ya kusema mimi hapa , au unataka nini kwangu? Ninatoroka kama Yona
ambaye hakutaka kufanya kile alichatakiwa na Bwana? Au ninafanya makusudi kufanya
Mapenzi ya Bwana kwa mtazamo wa kijuu juu tu , kama wale walimu wa sheria, ambao
Yesu aliwahukumu vibaya , kwani walikuwa wanafiki.Baba Mtakatifu anasema , kila kitu
sawa , hakuna maswali,na wala mimi sifanyi chochote zaidi au ninangali njia nyingine
kama walivyo fanya Mlawi na Kuhani mbele ya mtu masikini aliyejeruhiwa , na kupigwa
na majambzai , akaachwa nusu ya kufa. Jibu langu kwa Bwana ni lipi?
Aidha Baba Mtakatifu Francisko anasema : Bwana anapenda kubisha na sisi, akitoa mfano
juu ya hilo anafafanua na kusema, mtu anasema , Mimi Padre , mara nyingi ninapokweda
kusali ninapata hasira na Bwana, lakini hata hiyo ni sala, Baba Mtakatifu anasisitiza
na kuongeza, Yeye kwani anapenda anapoona kwamba umekasirika na unamwambia yeye uso
kwa uso kile ambacho unajisikia, kwasababu yeye ni Baba! Na hiyo pia ni jibu la “mimi
hapa. Alimalizia akisema akiuliza pia je mimi ninajificha , au ninajifanya manafiki,
au ninaangalia mahali pengine?Kila mmoja wetu wetu anaweza kujibu jinsi gani mimi
ninaitikia ndiyo mimi hapa , tayari kufanya mapenzi ya Bwana katika maisha yangu.
Na Roho Mtakatifu atupatie neema hiyo ya kupata jibu.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili, ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |