2017-01-24 16:50:00

Kanisa nchini Italia kuchangia milioni 22 kusaidia waathirika


Wito wa kujenga na kudumisha umoja ili kupunguza mateso ya wakazi waliothirika na tetemeko la ardhi , umakini kwaajili ya misaada ya kusaidia masikini,vilevile wasiwasi wa raia dhidi ya kipato kutokana na mapendekezo ya kisheria yaliyotolewa na serikali ya Italia. Hayo ni mawazo ya Kardinali Angelo Bagnasco, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia akitoa Hotuba yake kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Kudumu la Maaskofu Katoliki  wa Italia ulioanza tarehe 23 na utamalizika 25 Januari 2017.

Katika hotuba elekezi Kardinali anasema mtazamo wetu hauna budi kuanzia na matukio ya sasa yanayo endelea kujitokeza , ambayo kwa miezi hii umeathiri nchi ya Italia, na hivyo Kardinali anafungua kikao hicho kwa kutazama sehemu za Abruzzo, Lazio, Marche na Umbria ambazo zimeendelea na matetemeko ya ardhi na pia kuanguka kwa theruji nyingi  kusabisha  kazi kuwa ngumu ya kuokoa waathirika. Kwa njia hiyo Kardinali anatumia maneno kuwa yake ya Baba Mtakatifu Francisko wakati alipofanya ziara katika maeneo ya waliopata maafa ya tetemeko akisema  “Maparoko hawakuondoka  kuacha eneo “ Akiwa na maana ya kwamba watu wa kujitolea na vikosi vya wazima moto, pia jumuiya ya kikristo ,waliweza kufanya mshikamano na kuiwezesha Baraza la Maaskofu Katoliki wa Italia kuwa na kiasi cha Euro milioni 22 .

Fedha  hizo, zilizo kusanywa kupitia Caritas za kila Parokia nchini Italia ziliweza kununua mahitaji muhimu ya lazima.Na zaidi ya euro 300,000 ziliwekwa tayari kwa kila Jimbo la waathirika  kwaajili ya dharura ili kuweza kukarabati majengo ya Kanisa yanayotumika katika ibada na  kwa  vyumba vya mafunzo ya  huduma za kichungaji. Vile vile Kardinali Bagnasco anatumia maneno ya Rais wa Serikali ya Italia alipoomba umoja na uwajibikaji kwa ajili ya  kupoza mateso ya wanaoteseka, na wale walio athirika.kwasababu mawazo ya Rais wa Baraza la maaskofu wa Italia yanahusu hasa suala la umasikini na mazingira magumu yanayo endelea kuwakabili idadi kubwa ya wakazi wa Italia.Tangu mwanzo wa migogoro , watu walio na umaskini ziadi wamezidi kuongezeka  na kufikia  asilimia 55% na maelfu ya familia nyingi zimeweza kugundua mahali pa kupata majibu ambapo ni katika maparokia. Na kwa njia hiyo Kardinali Bagnasco anakazia umuhimu wa kuipa kipaumbele  kwanza ile sheria iliyonzishwa ya  kishirikishwa kwa mapato na mpango wa Taifa dhidi ya kupambana na umasikini.

Kardinali anatazama hali ya sasa kwa upande wa wakimbizi na hasa wale watoto wanaoingia  bila kisindikizwa na manyanyaso ,ki ukweli ni hali inayohusu changamoto kubwa ya dhamiri ya jamii nzima katika nchi na Taasisi zake kutafuta majibu thabiti. Kwa mtazamo huo ingekuwa muhimu kuwa na utambuzi wa uraia kwa watoto waliofika na kuanza shule ,na hata uwezekano wa kuwakabidhi watoto katika familia wale watoto wasio kuwa na wazazi,ni kutokana na kwamba inawezakana kabisa kwasababu ya  uzoefu wa mwongozi kutoka katika maparokia.Kwa mtazamo huo  Kardinali Bagnasco  anangalia mwaka wa neema ulio malizika hivi karibuni akisema kwamba maadhimisho ya Mwaka wa Jubilei kuu ya huruma ya Mungu umewafanya watu wengi kugeuka kuwa vyombo vya huruma.

Aidha aligusia kuhusu  matukio ya ukosefu wa  uaminifu kwa upande wa Wakleri na kusababisaha kashfa na kusema ni chanzo cha uchungu  , lakini pia haitufanya kushindwa kuheshima na kupongeza utume wa kikuhani kwa ujumla.Lakini anasisitiza kwamba ili kujirudi upya katika hali halisi ya ukuhani,ni lazima kuanzia katika mafunzo ya kudumu kwa lengo ka kuboresha wito kwa ujumla.Kwa kufanya hivyo hawali ya yote ni kuwa na mahusiano ya  kirafiki na Bwana, kwasabau hakuna mchungaji yoyote ambaye  hana  uhusiano binafsi na Yesu Kristo na kubaki naye .Moyo wa Mchungaji lazima ubaki na upendo wa kichungaji , ambao ni ushara ya kikuhani aliye wekwa wakfu  kuwa mbele ya Yesu mchungaji mwema.

Katika maandalizi ya Sinodi ya Maaskofu juu ya vijana itakayoadhimishwa kunako mwaka 2018   Kardinali anasema uso mzuri wa Kanisa unang’aa  na hasa zaidi kwa kutokana na kizazi kipya , kwa mwanga huo , Baba Mtakatifu amechagua Kauli mbiu ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana yenye kauli mbiu "Vijana, imani na mang'amuzi ya miito". Kwa mujibu wa Kardinali Bagnasco anasema ni vizuri kuwashirikisha vijana  maana yake kuwa nao karibu au kwa ajili yao vijana ni kutoa ushuhuda na sababu za maisha, kwa kuwavutia imani katika Yesu na kutafuta kujibu maswali yaliyo ndani kabisa ya ya mioyo yao ,ambayyo katika utamaduni wa sasa unaotawala unapenda  kusafisha na kuvuruga kuwalekeza barabara za uongo. Kardinali Bagnasco anamalizia akikumbuka kwamba siku siku hizi Kanisa  linaendelea kusali kwa ajili ya kuombea Umoja wa Wakristo hadi 25 Januari 2017, uwe umoja wa dhati ,na  ili ulimwengu upate kusadiki . Kwa maana hiyo, Kardinali anakumbuka ziara ya Kichungaji ya Baba Mtakatifu Francisko Huko Sweden juu ya Jubilei ya Miaka 500 ya Mageuzi ya Kiluteri Duniani, na hivyo anaitia moyo familia ya Mungu nchini Italia kufanya kila njia kupiga hatua madhubuti katika kukuza na kudumisha umoja wa Wakristo ndani na nje ya Italia.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.