2017-01-23 16:14:00

Sala ya Malaika wa Bwana:tupande mbegu ya Injili ili izae matunda


Injili ya siku ya Jumapili ya tatu ya Kipindi cha Mwaka A wa Kanisa imelezea juu ya mahubiri ya Yesu huko Galilaya. Aliacha Nazareth kijiji kilichokuwa katika milima kwenda Kafarnaumu, Njia hiyo ilikuwa moja maarufu kuelekea ziwa la Galilaya.Wakazi wa maeneo hayo walikwa karibu wote ni wapagani. Kuchagua kwenda huko  Yesu nataka kuonesha namna ya kwenda kuwahubiria hata watu wengine na siyo tu kuwahubiria watu wake kama ilivyokuwa imetabiriwa na Nabii Isaya (Is 8,23) kwamba hata Galilaya alitwa.Kijografia eneo hilo la pembeni lilijulikana kama la wapagani waliochanganyikana na waisraeli,na kwamba  kama Injili ya Jumapili iliyopita ilikuwa ikisema "watu walioshi gizani ndipo wameona mwanga" ni Mwanga wa Kristo hakika unaangazia hata pembeni.

Haya yamesemwa na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili, tarehe 22 Januari 2017 kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Baba Mtakatifu anaendelea kusema, utume wa Yesu unafanishwa na ule wa Mtakatifu Yohane mbatizaji aliyetangaza Ufalme wa mbinguni , japokuwa  ufalme haujikiti katikia mambo ya siasa na utawala wake , bali unajikita katika ukamilifu wa agano kati ya Mungu na watu ambao unatabiri kipindi cha amani na haki. Katika kukamilisha hilo agano la Mungu, kila mmoja amealikwa kutuvbu kuangoka , kubadilika namna  kufikiri  na jinsi ya  kuishi.Kuongoka siyo tu kubadili namna ya kuishi peke yake bali hata namna ya kufikiria. Mabadiliko ya kufikiria ni msingi kwa sababu hayatazami kubadilisha mavazi bali namna ya kuishi ukawaida , na ndiyo kinachotofautisha Yesu una Yohane Mbatizaji yaani  namna  na njia ya kuishi.

Yesu alichagua kuwa Nabii wa kutembea, yeye hakusubiri watu, bali aliondoka kwenda kukutana nao. Na daima amekuwa barabarani, na ndiyo maana safari yake ya kwanza ya kitume alionekana  kandokando ya ziwa la Galiya, na kukutana na umati wa watu hasa wavuvi.Yesu hakutangaza ujio wa ufalme wa Mungu tu bali alitafuta hata wafuasi wake ili waungane katika utume wa ukombozi. Na katika safari hiyo alikutana na ndugu wawili wawili  Simon  na Andra, Yakobo na Yohane, akawaita akisema , njoo  nyuma mnifuate nitawafanya wavuvi wa watu.Wito wake huo uliwakuta wakiwa katika kazi yao  ya kila siku: Kwa namna hiyo Bwana anatuonesha , anavyokuja kwetu siyo katika mambo ya kustaajabisha bali katika mambo yetu ya kawaida katika maisha yetu ya kila. Na hapo ndipo tunapaswa kumuona Bwana , na hapo Yeye anajionesha  na kusikika katika mioyo yetu. Ni pale katika mambo yetu ya kawaida ya kila siku  katika mazungumzo naye yanayobadili mioyo yetu.

Jibu la wavuvi lilikuwa tayari kumfuata  kwa haraka ,waliacha nyavu zao na kumfuata,tunatambua ya kwamba  Baba Mtakatifu Francisko anaeleza walikuwa ni wafuasi wa Yohane Mbatizaji, na kwaajil ya ushuhuda wake , walikuwa tayari wameanza kuamini Yesu ya kwamba ni Masiha (Yh1,35-42). Baba Mtakatifu anasema sisi kama wakristo leo hii tunapaswa kutanganza ushuhuda wa imani yetu iliyotangazwa kwa mara ya kwanza, na kwasababu walikuwawp wale watu wanyenyekevu na jasiri ambao waliitikia wito bila kujibakiza kumfuata Yesu .Ni pale kandokando ya ziawa , nchi ambayo haikufikiriwa, Lakini likawa eneo liliponzia Jumuiya ya kwanza ya utume wa Kristo.
Utambuzi wa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo utuamshe ndani ya mioyo yetu ule utashi wa kupeleka Neno la upendo na huruma ya Yesu katika kila sekta hata pale ambapo hapastahili.Kupeleka neno hata sehemu za pembezoni, ili kila eneo la dunia ipandwe mbegu ya Injili na iweze kutoa matunda.Na kwa maombezi ya Bikira Maria asaide kuitikia kwa furaha wito wa Yesu wa kutoa huduma ya ufalme wa Mungu.


BAADA YA SALA YA MALAIKA WA BWANA:

Mara baada ya mahubiri Baba Mtakatifu Francisko  aliendelea kuwakumbusha mahujaji wote ya kwamba tuko katika wiki ya kuombea umoja wa wakristo: kwa mwaka huu kauli mbiu  ni kutoka katika barua ya Mtakatifu Paulo inayotupatia mwongozo wa kufuata. “Upendo wa Kristo unatuwajibisha katika maridhiano”(2 Kor 5,14).Jumatano 25 Januari 2017 ni hitimisho la wiki ya maombi ya sala itakayofanyika kwa sala ya masifu ya Jioni katika Basilika ya Mtakatifu Paulo , ambapo wataudhuria ndugu wote kutoka makanisa na jumuiya mbalimbali za Kikristo zilizoko mjini Roma. Baba Mtakatifu Francisko aliwaalika kuendelea kusali ili utashi wa Yesu uweze kutimilika wa “ ili wote wae kitu kimoja” (Yh 17,22).

Aidha alikumbua tetemeko la Ardhi lililotokea tena hivi karibuni  na theruji iliyoanguka kwa wingi na kusababisha ndugu zetu wa maeneo  ya mikoa ya Abruzzo, Marche na Lazio kupata shida , na kwambaa yuko karibu nao kwa sala kuwaombea familia waliokumbwa na misiba ya kupoteza ndugu zao, Aliwatia moyo wanao endelea kwa ujasiri kukabiliana na theruji wakitafuta watu ambao bado hawajapatikana, na pia alitoa  wito kwa Kanisa mahalia waweze kuwasaidia watu waliopatwa na majanga hayo.Halikadhaliaka alikuwakumbuka watu wa Mashariki ya mbali na katika sehemu mbalimbali wanao tarajia kusherehekea mwaka mpya 28 Januari 2017, kwamba anawatakia baraka na hasa kwa familia kwamba waendlee kuwa ni shule ambamo wajifunze namna ya kuheshimiana, kuwasiliana na wengine na ndipo furaha inaweza kujaa tele ndani ya nyumba na kuwaangazia jamii.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.