Ujumbe kutoka kwa Maaaskofu wa shirikisho la makanisa Katoliki ya Ulaya , Marekani
na Afrika ya Kusini baada ya hija yao ya mshikamano katika nchi Takatifu kuanzia 14-19
Januari 2017, hija ya mwaka huu imewakilishwa na maaskofu 12.
Ujumbe unasema watu wengi katika nchi Takatifu wameishi maisha yao yote chini ya
utawala na ubaguzi wake , mgawanyiko wa kijamii lakini pamoja na hayo bado wanaendelea
kukiri imani yao kwa matumaini na mapambano kwaajili ya maridhiano.Kwa njia hiyo hawa
wanastahili leo na daima mshikamano wetu. Wajibu wao Maaskofu ni ule wa kuondoa
ujenzi wa kuta katika makazi ambayo ni ukiukwaji wa haki za wapelestina kwenye maeneo
kama vile Hebron na Yerusalem ya mashariki pamoja na kwamba imetambuliwa na Umoja
wa mataifa hivi karibuni na kusema kuwa kuna hali ya hatari ya ukosefu wa amani.
Hata hivyo uwajibikaji ni kutoa misaada kwa wakazi wa Gaza ambao wanaendelea kuishi
katika majanga ya kibinadamu yaliyotokana na binadamu mwenyewe , kwa miaka mingi wakiishi
kwa kuzingirwa pande zote na hasa uadui wa kisiasa uliosabishwa na ukosefu wa nia
njema ya pande zote zinazohusika .Kama Baba Mtakatifu Francisko anavyotukumbusha ya
kwamba watu wote tunapaswa kuwajibika ,kwa kuwatia motia moyo, katika kuhamasisha
kupinga vurugu ambayo imeleta mabadiliko makubwa ulimwenguni . Kwa maana ya kwamba
kuna ulazima wa kuwajibika mbele ua ukiukwaji wa haki msingi kama vile ujenzi wa
kuta za kutengenisha Palestina ikiwa pamoja na Bonde la Cremisan.
Wote kwa pamoja tunao wajibu wa kuhamasisha kwa kutafuta suluhisho kati nchi mbili
.Vatican ilisistitiza ya kwamba iwapo nchi ya Israel na Palestina hawatakubali kushikana
bega kwa bega , maridhiano kati ya viongozi wa ndani ya mipaka iliyo afikiana na
kujulikana kimataifa, amani hiyo itabaki kama ndoto ya mbali na pia usalama usio
kuwa na uhakika. Wote pamoja tunao wajibuwa kusaidia Kanisa mahalia katika mahitaji
yake kama vile Taasisi mbalimbali, mashirika yasiyo ya kiserikali, valantia, kwasababu
katika hali ngumu sana vyombo hivi vimeonesha ujasiri mkubwa katika kazi yao inayobadili
maisha.Imani yetu kwa Mungu inatupa matumaini,pamoja na ushuhuda wa wakristo wa Nchi
Takatifu tulio kutana nao na hasa vijana na watoto wametuhamasisha kufanya hivyo.
Ujumbe wao unamalizia kwa kusema , Biblia inatuambia hivi: “mwaka wa hamsini mtauheshimu
kwa kutangaza uhuru kwa watumwa , (Walawi 25:10).Kwa kipindi cha miaka 50 ya kutawaliwa
, ni lazima kuwaombea watu wapate uhuru wa kila mtu katika nchi Takatifu na kuwapatia
msaada wa vitendo na kufanya kazi kwa ajili ya mani na haki.
Waliodhuria hija Takatifu ni Askofu wa Declan Lang, Uingereza na Galles (Rais wa kamati ya maandalizi ya Hija nchi Takatifu),Askofu Stephen Ackermann, Ujermani, Askofu Peter Burcher, kutoka Mabaraza ya maaskofu wa nchi za Kaskazini mwa Ulaya. Askofu Oscar Cantú, Marekani, Askofu Christopher Chessun, Kanisa la Uingereza , Askofu Michel Dubost, Ufaransa, Askofu Lionel Gendron, Canada; Askofu Felix Gmür, Uswis,Askofu Nicholas Hudson, Kamati ya Mabaraza ya maaskofu wa shirikisho la Ulaya,Askofu William Kenney, Uingereza na Galles; Askofu William Nolan, Scotland .Wakisaidiwa na Munsinyo Duarte da Cunha, Baraza la maaskofu wa Ulaya na Padre Peter-John Pearson, Baraza la maaskofu wa Afrika ya Kusini.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |