2017-01-20 15:48:00

Shirika la wahamiaji na wakimbizi lazindua mpango mpya kwa mwaka 2017


Shirika  la wahamiaji na wakimbizi kwa kushirikiana na mashirika 72 wamezindua mpango mpya wa kukabiliana na hali halisi ya janga la  wakimbizi na wahamiaji  Barani Ulaya kwa mwaka 2017 Mpango huo katika maeneo ya kanda ni jibu  la kipeo cha wahamiaji na wakimbizi, kwa namna hiyo inayo dhamira ya kuimarisha nguvu za Serikali katika kuhakikisha mapokezi ya usalama kwa wale wanaoomba hifadhi na kulindwa kwa wahamiaji na wakimbizi. Mpango huo pia unataka kusaidia suluhisho kwa  muda mrefu ,katika kuendesha majengo na kulinda utu katika matukio ya wahamiaji, vilevile kwa mwaka 2017 watatoa kipaumbele cha uimarishaji wa ushirikiano na uratibu kati ya watendaji na wanaohusika.

Mkurugenzi wa Shirika wahamiaji kwa upande wa  Ulaya Bwana Vincent Cochetel alisema "kwa miaka miwili ya mwisho katika kukabiliana na suala la kuingia  kwa wahamiaji na wakimbizi  nchi za Ulaya zaidi ya milioni 1,3 katika nchi wamepata changamoto kubwa na kati ya changamoto hizo ni kwa upande wa ulinzi wa wahamiaji na wakimbizi.Mpango huo unawakilisha chombo madhubiti cha utendaji ambacho kitakuwa na wajibu wa  kuhakikisha operesheni ya kutosha  na kutoa jibu katika ushirikiano kwa kipindi cha mwaka 2017”.Naye msemaji wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji Bw.Leonard Doyle,  aliongeza "tuna wasiwasi hasa  kwa kwa upande wa mazingira  magumu  na mahitaji ya watoto , wanawake na wasichana, mpango huu unataka kutoa jibu kwaajili ya haja hiyo".

Hati ya mpango huo  inatoa mwongozo  ya kwamba kuna haja kubwa ya kutafuta ufumbuzi kwa kipindi kirefu kwaajili ya wakimbizi , na wahamiaji, ikiwa ni pamoja na mpango madhubiti wa ugawaji wa msaada kwa wale watakaorudi makwao kwa hiali yao na uimarishaji wa njia mbadala za kisheria kwaajili ya safari hatarishi , kama vile makazi mapya na kuwaunganisha na famila zao.Mkazo maalum zaidi ni kuweka kwenye mahitahiji maalumu ya wanawake na watoto wakimbizi na wahamiaji .Mpango huo ni pamoja na miradi ya majaribio kwa majibu ya kuleta ufanisi zadi kwa watoto yatima na wale wasio sindikizwa  ambao wako Ulaya,ambapo ni zaidi ya 25,000 ambao wamefika nchini italia kwa mwaka 2016 tu. Aidha Mpango huo pia unalenga kuimarisha hatua zenye lengo la kutambua na kuwasaidia waathirika wa unyanyasaji wa kingono na kijinsia.

Kutokana na haja ya kushughulikia si tu mahitaji ya watu hasa ambao wameshafika  bali pia hata kwa wale ambao bado wanahitaji kuingia Ulaya ki halali; halikadhalika mpango unatafakari pia hali ya kijiografia katika maingilio yanayofunika maeneo ya Uturuki , na mashariki ya mbali, Ulaya Kusini, Ulaya ya kati ,magharibi na Kaskazini.Na mwisho Mpango  huo unatoa  ufadhili jumla  dola za kimarekani milioni 691, kwa idadi ya watu wanaofikia 340,000 kwa mujibu wa watu ambao walikwisha tangullia na pia kwa  idadi ya watu waliokuwa tayari ndani ya nchi ambao wataendelea kupokea msaada kupitia mpango huo.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.