2017-01-20 14:48:00

Kard Onaiyekan anasema lazima kuungana pamoja kukomesha vurugu


Ni zaidi ya mwaka  mmoja umepita bila kuwa na taarifa za  Padre Gabriel Oyaka, mwanashirika wa wa Shirika la Roho Mtakatifu huko Nigeria , aliyetekwa nyara 7 Septemba 2015  huko Kogi .
Akiongea na Waandishi wa habari mara baada ya misa  ya kumbukumbu ya Padre aliyetekwa, Cardinali Olorufemi Onaiyekan, Askofu Mkuu wa Abuja, alikumbuka kwamba wateka nyara hawakusikika au kufanya mawasiliano  ya kutaka malipo ya fidia,hivyo ni juu ya mamlaka ya serikali kuwajibika kulinda maisha na mali za raia wa Nigeria na Kanisa haliwezi kufanya chochote zaidi ya kuiomba serikali kufanya kazi yake.


Aidha akizungumzia juu ya matukio kadhaa ya utekeji wa wazalendo wasio kuwa na hatia , wakiwemo kati yao mapadre, Kardinali Onayeiyekan anabainisha  kuwa “majanga haya yameandama nchi yetu, na jina lilaosikika sana ni wafugaji wa kabila la Fulani ambao wamekuwa wakijihusisha na mahuaji,  utekaji,na uhalirifu wa maisha na mali zao”
Wafugaji wa kabila  la Fulani wameshitakiwa mara nyingi kwa kushambulia vijiji kadhaa vya wakulima kwasababu ya hoja zao ya kuhamahama wakitafuta malisho mapya  ya mifugo yao.kwahiyo  Kardinali alihitimisha akisema "kwa mtazamo wangu, tunakabiliwa na dharura ya janga la Kitaifa  na kwa nchi nzima lazima kuungana pamoja kukomesha vurugu hizi. 

Sr Amgela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.