Wakristo wa sehemu zote za dunia wameanza sala ya kuombea umoja wa wakristo ulionza
Jumatano 18 Januari na unatrajiwa kumalizika tarehe 25, januari 2017 katika kilele
cha sikukuu ya kongoka kwa Mtakatifu Paulo Mtume na mwalimu wa Mataifa .
Maombi hayo kwa mwaka 2017 yameongozwa Kauli mbiu Upanisho: Upendo wa Kristo unatuwajibisha
ambapo viongozi wa wakuu wa Makanisa katoliki ya Umoja wa Ulaya wametoa ujumbe kutokana
na tukio hili wakisema hakika maneno ya Mtakatifu Paulo kwa wakorinto yanatuhamasisha
kusali kwaajili ya umoja wa wakristo.
Katika ujumbe wao wanasema historia ya Ukristo Ulaya imepitia katika kipindi kigumu
kilichosabisha mgawanyiko na hata hukumu na kutumia nguvu.
Aidha wanasema tukio la maombi ya sala kwa mwaka huu limeangukia wakati baadhi ya
makanisa wanajiandaa kusheherekea maadhimisho ya miaka ya 500 ya mageuzi na mwanzo
wa kiprotestanti.Tunapenda kukumbuka tena kipindi kigumu cha siku zilizopita kwa
sababu kufanya kumbukumbu ya matukio na kukabiliana historia yetu ni fursa ya pekee
yenye thamani katika kurudia kwa upya wajibu wetu wa kuponya majeraha na kushinda
mgawanyiko huo.
Na kwa hiyo tuelekeze mioyo yetu kwa Yesu Kristo, ambaye ni mpatanishi wa watu wote
na muumba na Mungu , ili atuongoze katika kutekeleza wajibu huo.Ni kwa njia ya unyenyekevupia
shukrani tulizopewa tufanye mapatano kwa njia ya maneno na matendo yetu.Leo hii tunaadhimisha
tulivyo komaa na kujifunza kushirikiana kazi kwa pamoja, juu ya mazungumzo taalimungu.Aidha
ujumbe unasema; Viongozi wakuu wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki wa Ulaya, tumekuwa
tukishirikiana kwa miaka 45 kwa pamoja katika masuala kadhaa yenye maslahi ya pamoja,ni
pamoja na kushirikishana mateso na furaha za dunia inayotuunganisha.
Ujumbe unataja baadhi ya shughuli za pamoja ;mshikamano wetu na watu wote ,hata watu
wasio kuwa na kabila (ROM), juhudi zetu kwa upande wa haki na amani na mazingira,
maombi kwa anjil ya umoja wa ndani katika mwilisho wa Kristo ,ni mambo yaliyo tutia
nguvu katika mahusiano yetu.
Pamoja na yote zipo hata changamoto wakisema, migogoro mingi ambayo Ulaya na nchi
za jirani tumeitwa kukabiliana , ni muhimu zaidi kwani vita, na migogoro , kutokuwa
na uhakika wa kisiasa , uhamiaji na changamoto ya mazingiria, umasikini wa mali na
wa kiroho, vina athiri maisha ya kila mtu katika nchi za Ulaya na kwingineko lakini
pamoja na migogoro hii yapo pia matumaini. Kwa njia hiyo tunaweza kushuhudia upendo
wa Kristo kwa maridhiano kupitia uadilifu na kazi ya uumbaji , mshikamano dhidi ya
maskini na ulinzi wa heshima ya watu wa Mungu.
Hitimisho la ujumbe; kwa upande wetu tunapaswa kuimarisha zaidi njia ya mazingumzo
kwa pande zote. Kwa njia ya shuhuda na matendo tujenge madaraja, kwa njia ya maombi
tujifunze kutambua kazi ya Roho Mtakatifu .Njia ya kufuata yawezekana kuonekana ni
rahisi, lakini cha muhimu ni kukazia ukweli wa maneno haya ya “upendo wa Kristo
unatuwajibisha”.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |