2017-01-18 15:54:00

Simameni kidete kulinda imani na kuwahudumia maskini!


Vatican inapenda kuungana pamoja na kuwatia moyo wanachama wa Shirika la Kijeshi la Malta wanaotekeleza dhamana na wajibu wao sehemu mbali mbali za dunia kama sehemu ya mchakato wa kulinda imani na huduma kwa maskini, wagonjwa na wahitaji zaidi. Hii ni sehemu ya ujumbe uliotolewa na Vatican kuhusiana na matukio kadhaa yaliyotikisa Shirika la Kijeshi la Malta, kiasi cha Baba Mtakatifu Francisko kulazimika kuunda tume ya watu watano hapo tarehe 21 Desemba 2016 itakayochunguza matukio haya na hatimaye, kumpatia taarifa kamili.

Vatican katika taarifa yake kwa vyombo vya habari inasema, ina imani na wajumbe walioteuliwa na Baba Mtakatifu kufanya uchunguzi wa kina kwenye Makao Makuu ya Shirika hili na inakataa kukubaliana na taarifa za kutaka kupaka matope kazi za Shirika hili, kutokana na nyaraka mbali mbali ilizo nazo!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.