Katika kuadhimisha sikukuu ya mashahidi wa Uganda kila ifikapo tarehe 3 Juni ya
Kila mwaka, Kwa mwaka 2017 Baraza la Maaskofu wa Uganda wamechagua kauli mbiu itakayoongoza
siku hiyo kwamba “ kuweni imara katika imani kama mlivyofundishwa.” Aliyatamka hayo
Askofu Vincent Kirabo wa Jimbo la Hoima kwa siku zilizopita kwamba kauli hiyo imechaguliwa
kutoka katika Barua ya Mtakatifu Paulo kwa Wakolosai (Kol 2,7)
Muhusika wa maandalizi ya tukio Emmanuel Kiiza Aliba alisema ;kauli mbiu hiyo inajikita
katika ushuhuda mkubwa kwa waamini wanao paswa kuutoa kwa Kristo, mtu binafsi, katika
familia, katika maeneo ya kazi na kwa sehemu zozote ambazo tunakuwapo. Pamoja na hayo
katika sikukuu ya mashahidi wa Uganda itakuwa na maana kubwa kwa Jimbo la Hoima kutokana
na kwamba mwaka jana 2016 Jimbo lilisherehekea miaka 100 ya uinjilishaji na kwa mwaka
huu wanategemea kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 52 ya kuundwa kwa jimbo. Aliongeza
Aliba tumekomaa kiimani , na sasa tunapaswa kutafakari kwa kina Injili.
Kwa kawaida sikukuu ya Mashahidi wa Uganda , ufanyika kila tarehe tatu ya mwezi wa
sita, na sherehe hizo ufanyika katika Madhabau ya mashahidi Namugongo, kwa njia hiyo
maandalizi ya mwaka huu yanatarajiwa kuanza na sala ya Novena.Mashahidi wa uganda
kwa ujumla ni 45 wakiwa ni wakatoliki na wangilikani.
Mfiadini wa kwanza anayejulikana sana ni Mtakatifu Carol Lwanga,kwani yeye na wenzake
waliuwawa kinyama kwa kutetea imani yao chini ya utawala wa kifalme wa Mwanga (1884-1903);Na
kifo chao kilitokea kati ya Novemba 1885 - 27 Januari 1887. Tarehe 6 Juni 1929 walitangazwa
kuwa wenye heri na Baba Mtakatifu Benedikto wa XV; na tarehe 8 Oktoba 1964 wakatangazwa
watakatifu na Baba Mtakatifu Paulo VI.
Ikumbukwe Novemba 2015 katika safari yake ya kitume huko Afrika , Baba Mtakatifu
Francisko alielekea katika madhabahu ya Namungongo Uganda , wakati wa mahubiri yake
alisema kwamba kurithi mashahidi wa Uganda, ni kurithi maisha yaliyo ongozwa na nguvu
ya roho Mtakatifu na kwamba ni maisha yanayo toa ushuhuda hata sasa katika kuleta
nguvu ya mageuzi ya Injili ya Yesu Kristo.
Halikadhalika alisema; ”hatuwezi kutunza urithi huu kuwa kumbukumbu ya kawada au kuhifadhi
hiyo kumbukumbu katika jumba la makumbusho kama kito cha thamani, bali tuna heshimu
kweli, na kuwaheshimu watakatifu wote,na zaidi ni kuleta ushuhuda wao wa Kristo katika
nyumba zetu, kwa jirani zetu, katika sehemu za kazi , na katika vyama vya kijamii,ushuhuda
huu uwe katika nyumba zetu, na hata mahali popote tutakapo kwenda pembe za dunia.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |