Katika siku ya wiki ya 12 ya sala kwaajili ya amani , ifanyikayo kila mwaka jimbo Kuu la Gulu Uganda ,Askofu Mkuu John Baptist Odama na Rais wa Baraza la Maaksofu Uganda , alitoa wito kwa watu wote juu ya kuhamasisha amani badala ya wale wanatetea virugu . Aliwakaribisha watu wote waweze kufanya mazungumzo ya amani badala ya maongezi ya uchochezi kwasababu ya kusaidiana kuleta amani kwa wote.Gazeti la Fides limemnukuu akisema, "naomba kila moyo usiwaze vurugu, wala kuchochea vurugu na kadhalika kila juhudu za mwili zisihamasishe vurugu".
Makutano hayo ya sala yalianza tarehe 9 -13 Januari 2017 Mahujaji wa amani zaidi
ya elfu tano walipata kuudhuria kutoka pande za kaskazini mwa Uganda, kusini mwa Sudan,na
pia wengine kutoka jimbo kuu la Gulu katika majimbo ya Nebbi , Arua na Lira.Kauli
mbiu ya siku hiyo ilikuwa kama ya Baba Mtakatifu Francisko aliyoichagua katika sala
ya amani kwa dunia nzima kwa mwaka huu 2017 yasemayo "Kutokutumia nguvu: mtindo wa
siasa ya amani”; ambapo anawaalika binadamu wote kutokutumia nguvu na kuhamasisha
amani.
Monsinyo Odama aliwageukia kwa namna ya pekee mahujaji , akiwataka wasali kwa ajili ya nchi na kwa ulimwengu , ambapo bado kuna migogoro ya kivita ,kama vile Sudan ya Kusini, Somalia, Afghanistan, Syria, Iraq, Mali, Libya, Yemen, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) , Jamhuri ya Afrika ya Kati (RCA), Nigeria, Gambia na Uganda.Aidha Askofu Mkuu aliwataka viongozi wote wa dini kuzingatia suala la amani ambapo yeye mwenyewe amekuwa na jukumu muhimu katika hitimisho la miaka ishirini ya vita kati ya vikosi vya serikali , na chama cha upinzani (LRA) Kaskazini mwa Uganda.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |