Changamoto, fursa zaidi, na zaidi ya yote ni ushuhuda wa ukaribu wa Kanisa kwa
watu. Hiyo ndiyo ilikuwa kazi ya upatanishi uliyofanywa wiki za hivi karibuni katika
nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Hayo yalisema na Askofu Nicolas Djomo Tshumbe
Rais wa Zamani wa Baraza la Maaskofu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alipohojiwa
na Gazeti la Osservatore Romano, kuelezea namna ya Kanisa likmukuwa kati yao katika
kuelekea uchaguzi mkuu nchini humo.
Anasema kwamba wakati wakuu walifanya mkutano wao huko Angola mwaka jana Oktaba 2016
kwenye Mkutano ulioitishwa na mkutano wa Kimataifa wa kanda ya maziwa Makuu, Umoja
wa Mataifa, na mashirika mengine ya mikoa, wali mshauri Rais Joseph kabila , kuteua
wapatanishi kutoka Baraza la maaskofu , kwa kuzingatia ushawishi wa Kanisa , uhusiano
wake na wadau wa kisiasa , na zaidi ya yote uwepo wake katika kijikita kwenye masuala
msingi ya jamii.
Kwa jinsi hiyo nasema "tuliweza kuzingatia na kufanya mazungumzo kwa pande zote mbili
zenye migogoro: sehemu ya mashirika ya kiraia na sehemu ndogo ya wapinzani, na wengine
wengi walio katika upande wa Rais". Aliendelea; “tulikutana kwenye wiki za hivi karibuni
kwa pamoja na wadau wa sera zote za kisiasa: wanachama wa upinzani,na wale kwa upande
wa Rais;kutokana na kuamini Kanisa, wote walipata kuitikia wito wetu , na kujadili
kwa wiki tatu katika maelewano ya kisiasa, hadi kufikia makubaliano ambayo yataruhusu
sera zote mbili za siasa kutawala nchi pamoja mpaka uchaguzi ujao.Aidha anasema pamoja
na hayo yote kuna kipengele kilicho muhimu sana cha makubalianao ya kwamba Rais Kabila
hataweza kugombea kwa hawamu ya tatu bali ataendelea kutekeleza majukumu yake hadi
uchaguzi ujao,kwa dhana kwamba ni kuhakikisha ,unakuwepo mwendelezo wa serikali kwani
katiba ya nchi inaruhusu. Hata hivyo Kabila alijitahidi kutokufanya marekebisho ya
katiba,kuhusu kura za maoni au utaratibu wa bunge wala wakati wa kipindi cha usimamizi
shirikishi. Hii imepunguza mvutano kati ya idadi ya watu na kurejea kwa matumaini
dhidi ya mabishano makubwa ya kisiasa.Hiyo ni hatua muhimu ya makubaliano, kwa wakati
wa wiki hizi ambapo tuko katika kazi juu ya sheria utekelezaji.
Kuhusu majadiliano yao ya kikao hicho Askofu anasema kwamba : katika hatua hizo za muda , inahusu kufanya majadiliano ya Waziri mkuu , ambaye anapaswa kuwa msimazii wapande zote za upinzani, kuzungumzia juu ya ukubwa wa Serikali ambayo ataingoza kuelekea uchaguzi.Inabidi kufikia uamuzi katika ya mgawanyiko uliopo na majukumu kati ya vyama.Aidha anabainisha kwamba inabidi kuzungumza katika Baraza la taifa kwa kufuatilia makubaliano, mengine ni kusubiri muda itakapofika uteuzi wa Waziri mkuu , wakati serikali itakapopitisha bunge. Akaongeza kwamba walichokifanya ni kuwaomba wapate ufumbuzi wa haraka iwezekanavyo .”Tunapaswa kufikia makubaliano haraka iwezekanavyo”.
Aidha alisema, kwamba anamshukuru Baba Mtakatifu Francisko , kwa sababu yeye amesaidia wao tangu mwanzo . Kwani tarehe 19 Desemba mwaka jana ,walikutana na baraza la maaskofu wa Congo na waliwatia moyo katika kazi ngumu wanayo kabiliana nayo.Kwa hali halisi kweli bado hali ni teta sana , kwani hata vikosi hivyo vya kisasa vinatuomba tuendelee kuwasindikiza katika mchakato wa kisiasa.Inabidi kuandaa hadi kufikia uchaguzi pamoja na matatizo yote yatakayojitokeza.Kama nilivyokwisha kusema, kwamba sekta za wanasiasa , wametuomba kwa matumaini tuwasindikiezikize na hili kwetu ni fursa ya kweli na inayoleta matumaini.
Afrika inaweza kuondoka na migogoro kwa wakati ujao? Askofu anasema , migogoro inaletwa
na sababu mbalimbali. Katika ukanda wa Maziwa Makuu, mara nyingi ni sababu za kiuchumi
na katika nchi yetu,Lakini sababu nyingi zinajihusishwa na kunyonywa kwaajili ya madini
,hasa katika ukusanyaji wa madini muhimu yenye thamani yenye kutengeneza wa Kompiuta.Ni
lazima kulenga sera za wanasiasa wakawa na moyo wa kujikita zaidi katika maslahi
ya pamoja na siyo tu ya binafsi, na hiyo inawezekana kwa njia ya kuelimshwa. Ni lazima
kuwa na wanasiasa waaminifu na wenye uwezo wa kufanya kazi kwa ajili ya nchi yao
na jamii zao na si kwa ajili ya manufaa binafsi. Hiyo ndiyo njia pekee ya kufikia
hali halisi ya sheria. Na kwa namna hiyo tunaweza kupata mfumo ambao ni wa kulinda
watu walio dhaifu na wanaoishi katika mazingira magumu, hasa wanawake na watoto. Kwa
kifupi, ingekuwa vizuri kufuata mafundisho ya kijamii ya Kanisa, na kwa pamoja tukafanya
kazi katika mwelekeo huu kwa ajili ya baadaye na kujenga jamii mpya ya Congo.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |