Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 14 Januari 2017 amekutana na wajumbe wa "Global Foundation na kutoa hotuba yake akisema , anayo furaha kwaajili ya meza yao ya mduara ya chama hicho cha " Roma Global Foundation", ikiongozwa na kauli mbiu inayaofanana na chama chao “kwa pamoja tujibidishe kwa manufaa ya ulimwengu” ili kuweza kugundua njia rahisi ya kuweza kuwafikisha kwenye utandawazi wenye muungano chanya,tofauti na utandawazi wenye utofauti.Nia kubwa ni kuhakikisha kwamba jumuia zote zilizoundwa, taasisi,na mashirika katika jamii waweze kufikia malengo ya kimataifa yaliyo kubaliwa kwenye ajenda ya 2010 ya maendeleo endelevu
Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa kuna aina ya mifumo isiyokubalika , mifumo ya kiuchumi ambayo inatupilia mbali watu kwa kwa madai ya kwamba hawa hawaonekani,na hata kuleta faida kulingana na vigezo vya faida ya makampuni au mashirika mengine.Tofauti hizo husababisha wengine kunyimwa haki msingi za kiutu hasa katika mifumo ya kisiasa na kiucumi.Wale wenye kusababisha au kuruhusu tofauti ya wengine hawajali wakimbizi, unyanyasaji wa watoto, maskini wanao kufa kwenye mitaa na barabarani wakati wa baridi .Hata hivyo Baba mtakatifu Francisko anasema wanao sababisha hayo ugeuka kuwa kama mashine zisizo kuwa na roho kwa kukubali kanuni hiyo lakini mapema au baaye, hata wao watakuja kubaguliwa watakapokuwa hawana manufaa tena katika jamii ambayo iliwazesha kuweka kipaumbele fedha zao.
Mwaka 1991, Mtakatifu John Paul II, wakati wa kuanguka kwa mfumo wa ukandamizaji wa kisiasa na kutokea maendeleo ya ushirikiano wa taratibu za masoko ambayo tunaweza kusema ni ya utandawazi, alihisi hatari ambayo ingeenea popote na hasa itikadi za kiuchumi.Kwani hizo zingesababisha kidogo au bila kujali matukio ya kubaguliwa , unyonyaji na kutengwa kwa binadamu, na kupuuza wengi wanao ishi katika hali ya umasikini unaokithiri, unyanyaso, na upofu wa kuwakabidhi suluhisho pekee kwa maendeleo katika nguvu za masoko.
Kwa bahati mbaya , hatari aliyo kuwa ameona Mtakatifu Yohane Paulo II kwa kiasi kikubwa imejitokeza.Pamoja na hayo yote lakini,zimejitokeza juhudi za maendeleo kutoka kwa watu binafsi na taasisi ya kutuliza tahabu, ubaya na mateso yaliyo tokana na utandawazi usio wajibika. Alitoa mfano wa juhudi hizo kwa ushuhuda wa Mama Teresa wa Kalcutta , ambaye yeye mwenyewe alipata furaha ya kumtanganza Mtakatifu miezi michache iliyopita na mbaye ni ishara ya nyakati zetu, kwa namna fulani, aliwakilisha jitihada hizo.Baba Mtakatifu Francisko anasema yeye aliinama na kuokoa watu walio kuwa wameachwa pembezoni mwa barabara wakiangaika au kufa, kwa kutambua kila mmoja utu wake aliopewa na Mungu.
“Yeye alikaribisha maisha ya kila mwanadamu, ambaye hajazaliwa , na yeye aliyekuwa
ametupwa kwenye takataka, aidha, yeye alifanya asikike sauti yake kwa watawala wa
nchi, ili wapate kujua uhalifu na umasikini ulio sababishwa na wao wenyewe”.( Mhubiri
ya Baba Mtakatifu kwa tukio la kutangazwa mama Teresa wa Kalcutta 4 Septemba 2016)
Baba Mtakatifu Francisko anasema hii ni tabia ya kwanza ambayo inaweza kusababisha
utandawazi wa mshikamano na vyama vya ushirika. Ni muhimu, hawali ya yote kwamba kila
mtu, binafsi, asiwe tofauti na majeraha ya masikini, bali ajijfunze kuteseka na wale
ambao wanakabiliwa na mateso, upweke, kukimbia kwa kulazimishwa au kutengwa na familia
zao; pamoja na wale ambao hawapati huduma za afya pamoja na wale wenye njaa na baridi
au joto.
Huruma hii itahakikisha kwamba wanaondesha sera za kisiasa na kiuchumi wanaweza kutumia
akili na pia rasilimali zao siyo tu kuthibiti na kufuatilia athari za utandawazi,
bali wapate kusaidiwa kwa njia ya sekta mbalimbali za kisiasa , mikoa , taifa na kimataifa,
kuwasahihisha kwa kuwapa mwongozo kila inapobidi.Baba Mtakatifu aliongeza ; Siasa
na uchumi, kwa hakika wanapaswa kutambua zoezi hili la wema na busara.
Kanisa daima lina amini, Baba Mtakatifu Francisko anasema kwasababu linajua uwezo mkubwa wa akili ya binadamu ambaye daima ukubali asaidiwe na kuongozwa na Mungu,na hata utashi mwema walio nao wadogo na wakubwa kama vile masikini , matajiri, waajiri na wafanyakazi.Wito wake baba Mtakatifu ni kuwatia moyo waendele na ahadi yao inayoongozwa daima na mafundisho ya Kanisa, wakihamasisha ule utandawazi katika vyama vya pamoja na wadau wote husika kama vile , vyama vya kiraia, serikali, mashirika ya kimataifa, kitaaluma,kisayansi jamii na wengine . Alimazia hotuba yake akiwatakia matashi mema ya kazi zao.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |