Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 13 Januari 2017 amekutana na vikosi vya ulinzi na usalama vinavtoa huduma yake mjini Vatican ili kutakiana kwa salamu na matashi mema ya mwaka mpya wa 2017 kama ilivyo utamaduni wao wa kukutana nao kila mwaka. Akianza na salamu kwa niaba ya wote, Kamanda wa ulinzi na usalama wa Italia katika mji wa Vatican Maria Rosaria Maiorino, alisema anayo furaha ya kumsalimia kwa niaba ya wote ikiwa ni ratiba yao ya kila mwaka kukutana naye,na kwa upande wake akisema ni shahuku kubwa kama kamanda wa kikosi cha ulinzi wa raia katika mji wake.
Aidha alisema natoa salama na matashi mema ya mwaka mpya ambao umeanza hivi karibuni kutoka kwa Kamanda Mkuu wa Polisi , na Mkurungenzi Mkuu wa Ulinzi na usalama wa raia Bwana Franco Gabrielli, ambaye hakuweza kufika kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika,pamoja na hayo amewakilishwa na Kaimu wake Bwana Luigi Savina, Mkuu wa Polisi Gianfelice Bellesini, Padre anayetoa huduma katika Kanisa lao, na mapaolisi wote wa Ulinzi wa Taifa kwa uapande wa Vatican waliokuwa wameshiriki katika mkutano huo."Na kwa namna ya pekee, ninapenda kutoa salama zangu za dhati kwa walinzi wa usalama wa papa kutoka Uswis na walinzi wa usalama wa Vatican,ambao wamekuwa nasi bega kwa bega katika shughuli za ulinzi na usalama kwa dhati ni marafiki wa kweli". Alisema Kamanda Maiorino.
"Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu ulio malizika muda mfupi ni mamilioni
ya watu walifika kutoka pande zote za dunia, ili kuingia katika nyumba ya Mtakatifu
Petro, kusikiliza maneno yako.Kwa upande wetu wa ulinzi na usalama , ilikuwa mwaka
wa shughuli kubwa ulikuwa umejaa matukio mengi, lakini tuliweza kufanya kazi kwa utulivuna
kwa kutiii kanuni ya Mtakatifu Benedikto ambayo ina shirikisha mambo yote mawili ya
kazi na sala.
Wito wako wa kila siku Baba Mtakatifu,juu ya msingi wa maisha ya binadamu, kama vile
msamaha, maridhiano, na upendo ni vitu ambavyo vimekuwa , msingi na nguzo yetu ya
kusimamia kidete katika shughuli za kila siku na wenzangu tunao shirikiana pamoja
katika kazi na pia katika kutunza familia zetu.
"Tumeishi kipindi cha Jubilei ya huruma ya Mungu kama fursa ya kukua kiimani na
imetuwezesha kufanya kazi bila kuchoka kutokana na na kusikiliza wito wako wewe Baba
Mtakatifu wa kutuhimiza tuwe chombo cha maridhiano na kuwa wajenzi wa madaraja,pia
kupanda mbegu za amani".
Halikadhalika anasema, "kwa sasa tunaishi kipindi kigumu kisicho kuwa na uhakika,
kutokana na hali ya kutaka kwenda kinyume na maadili , yaani kwa mtazamo wa dunia.
Lakini kwa wito wako wenye nguvu umetuhimiza na kutuamsha tuendelee na shughuli zetu
kwa kuhakikisha kwamba ulinzi na usalama wa raia unaedelea kuwepo daima , tukiutenda
kiustadi na uwajibikaji,vilevile kuwa na subiria ya kila siku kwa ajili ya wote, watalii,
waamini na mahujaji wote. Alimalizia akisema "tuinue mioyo yetu pamoja na kutamani
huruma ya Mungu ili atuzidishie kuwa na imani ya kweli katika kuhamasisha amani ,
ukweli upendo na uhuru.Na kwa maneno hayo ninajiweka mikononi mwako tukiwa na matumaini
ya kupata baraka kwa wote , kwaajili ya familia zetu na kwaajili kazi zetu.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |