2017-01-11 15:45:00

Vatican: Kampeni kwa njia ya mitandao kuhusu wahamiaji na wakimbizi


Kutokana na tukio la Siku ya wahamiaji na wakimbizi duniani itakayofanyika 15 Januari 2017, Kamati ya Baraza la wahamiaja na wakimbizi Vatican, kwa ajili ya Huduma ya maendeleo ya kibinadamu na imezindua kwa mara ya kwanza, Kampeni kupitia vyombo vya habari na mitando ya kijamii , ili kuongeza uelewa , juu ya suala hili ambalo liko ndani ya uwezo wake.


Kampeni hiyo znakwenda sambamba na kaulimbiu iliyo chaguliwa na Papa kwa mwaka 2017 juu ya Siku ya wahamiaji na wakimbizi hasa  kwa upande wa ( watoto,wahamiaji na wanaoishi katika mazingira magumu na hawana sauti.)

Hivyo Kampeni hiyo ya mitandao italenga hasa hali ya watoto , vijana na wahamiaji, wakimbizi , msongamano na waathirika wa biashara haramu ya binadamu. Kuanzia tarehe 12 hadi 15 Januari 2017 tweet zote za Vatican, zitagusia juu ya suala hili na watatuma ujumbe moja kwa moja katika mitandao ya facebook.Na ujumbe huo utakuwa una onesha historia fupi na tafakari juu ya suala hili.


Atakaye penda kufuatilia , anuani za mitandao ya kijamii zimetolewa:
Twitter Accounts:

English - https://twitter.com/M_RSection
Italian - https://twitter.com/M_RSezione
Spanish - https://twitter.com/M_RSeccion
French - https://twitter.com/M_RSection_Fr
Facebook: https://www.facebook.com/MandRSection/
LinkedIn: https://www.linkedin.com/company/migrants-&-refugees-section


Tunawaalika kufuatilia katika mitandao ya kijamii na kuwasambazia habari njema wenzenu na marafiki .
Na kwa maelezo zaidi wasiliana na Lidia Magni,
lmagni@mrsection.org

 

 

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.