2017-01-11 15:30:00

Papa Francisko: Epukeni matapeli!


Baada ya katekesi Baba Mtakatifu Francisko aliwasalimia mahujaji wote waliofika katika ukumbi wa Paulo wa VI kwa lugha mbalimbali, akitoa salamu kwa namna ya pekee kwa mapadre, walimu wanaofundisha katika seminari Kuu na vyuo mbalimbali vinayoshirikiana na chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana Roma, Chama cha mpira “Fidelis Andria” na vijana wa Chuo cha ufundi Caetani ya Cisterna huko Latina Italia, aliwataka wote watende vema shughuli zao za kitume kwa moyo na  unyenyekevu kwa ndugu na jirani zao.

Kwa kuchekesha watu lakini ni ukweli, Baba Mtakatifu aliwambia watu ya kwamba kuna tiketi za kuingia bure Vatican ma katika ukumbi kusikiliza katekesi lakini cha kushangaza wapo watu wajanja wanao chukua tiketi na kuziuza, hivyo aliwaonya,na kusema “ hizo tiketi zinatolewa bure  na siyo za kununuliwa , ni Papa ametengeneza kwa ajili wageni, na hivyo hakuna mtu auze hizo tiketi mmeelewa?... Watu wote  walipigia makofu kwa kushangilia….Kuweni makini na hao wezi wanaotaka kuwaibia...,kwasababu hii ni nyumba ya wote na wanaingia watu wote. Aliendelea na salam zake kwa vijana wote, wagonjwa na  wana ndoa.Na kusema pia kwamba “Jumapili iliyopita ilikuwa ni sikukuu ya Ubatizo wa Bwana, kutokana na tukio hilo limetufanya kufirikiria upya juu ya ubatizo wetu katika imani ya Kanisa"

Aidha kwa vijana alisema”Vijana gundueni kila siku neema itokanayo na Sakramenti mliyoipokea; na upande wa wagonjwa Baba Mtakatifu Francisko alisema; “Na nyinyi wagojwa , choteni nguvu itokanayo na ubatizo ili kukabiliana na uchungu na  kukata tamaa. Na mwisho Baba Mtakatifu aliwageukia wana ndoa wapya akisema; “tambueni namna ya kuwajibisha utabitìzo wenu kwenye matendo katika njia yenu ya maisha ya familia.

Sr Angla Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.