2017-01-10 11:17:00

Nchi za Kiafrika kukutana Brazzaville, 25 Januari ili kujadili Libia


Bwana Jean Claude Gakosoo, Waziri wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa nchini Congo Brazzaville amesema, tarehe 25 Januari 2017 kutafanyika mkutano  utakaowahusisha wawakilishi wa nchi za Kiafrika ili kujadili kwa kina na mapana machafuko ya kisiasa nchini Libia, ili hatimaye, kuweza kufikia ufumbuzi wa kudumu. Machafuko ya kisiasa nchini Libia yanapaswa kufikia ukomo wake kama sehemu ya mchakato wa kujenga na kudumisha haki, demokrasia umoja na mshikamano wa kitaifa.

Tayari Algeria nchi ambayo inapakana kwa karibu zaidi na Libya imeonesha kuunga mkono juhudi za Congo Brazzaville ili kuendeleza mchakato wa umoja na maridhiano ya kitaifa yaliyopelekea kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa chini ya Rais Fayez Al Sarraj.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.