2017-01-09 15:50:00

Papa Francisko: Jitahidini kumfahamu, kumwabudu na kumfuasa Kristo!


Maisha ya Kikristo ni rahisi na wala siyo mahitaji ya kitu ambacho ni cha  kustajabisha  au kigumu, bali ni kuweka Yesu mstari wa mbele kwenye uchaguzi wa maisha yetu ya kila siku. Ni maneno yake Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Mahubiri ya Jumatatu 9 Januari 2017 wakati Kanisa linaendelea tena na Liturjia ya  kipindi cha kawaida cha mwaka baada ya sikukuu za Krismasi kuisha katika Kikanisa cha Mtakatifu Martha mjini Vatican.

"Baada ya kuzaliwa kwa Bwana , tunaanza upya liturujia ya kawaida ya kipindi cha mwaka" ,Papa alisema  lakini katikati ya maisha ya kikristo yupo Yesu daima,aliye wa kwanza na mwenye  neno la mwisho la Baba, Bwana wa Ulimwengu, mwokozi wa Dunia. Na hakuna mwingine yoyote bali yeye peke yake".  "Yesu Kristo ndiye kitovu cha maisha yetu. Yesu Kristo aliyejionesha na anaonekana , nasi tunaalikwa kumjua katika maisha yetu, na katika matukio yoyote ya maisha yetu, ni kumjua  Yesu". Papa alisema.

Alitoa mifano Baba Mtakatifu alisema, "wengine wanamwambia; mimi Padre, nina fahamu maisha ya mtakatifu huyo au yule au kutokea kwa Bikra Maria hapa na pale, ndiyo hayo yote ni mema , watakatifu ni watakatifu kweli na ni wakubwa!,  lakini matokeo ya Bikra Maria siyo daima ni ya kweli; alisisitiza , watakatifu ni muhimu lakini kitovu cha hayo yote ni Yesu Kristo: kwasababu bila uwepo Yesu Kristo  hakuna hata watakatifu! Na ndipo swali la kujiuliza linakuja :Je kitovu cha maisha yangu ni Yesu kristo?  Je uhusiano wangu na Yesu Kristo ukoje?"

“Kuna mazoezi matatu “ili kuhakikisha ya kwamba Yesu ni kitovu cha maisha yetu” Baba Mtakatifu aliendelea na mahubiri yake akisema “ Zoezi la kwanza ni kumjua Yesu ili kumtambua kiukweli.Kwa  nyakati zake , watu wengi hawakumtambua Yesu ni nani” Akatoa mifano kama vile; “ walimu wa sheria, makuhani waandishi , masadukayo na baadhi ya malifasayo”.Zaidi ya hayo papa alisema “walimsonga hadi  wakamuua : na hivyo inabidi kujiuliza je kuna haja  kwangu kumfahamu Yesu? , au labda nina haja ya kuangalia picha za simulizi,  au hamu ya kutaka kujua habari za wengine?. Alielezea Papa Francisko ,” ili kumtambua Yesu , kuna sala ya Roho Mtakatifu”, lakini pia kuna Injili ambayo mnapaswa kwenda nayo  na kuisoma kurasa kila siku. Hiyo ndiyo njia ya kumjua  Yesu. Zaidi ya hayo ni roho mtakatifu anayefanya kazi yake baadaye, na hiyo ndiyo mbegu.Anayefanya mbegu ikue ni Roho mtakatifu.

Zoezi  la pili ni  kuabudu Yesu.Siyo tu kuomba vitu na  kushukuru, bali ni sala ya  kuabudu kwa ukimya  na pia kujing’uta yote yaliyo ndani ya mioyo yetu hasa  yale ya malimwengu tunayoyasifia zaidi, ni kuyatoa nje   na kuabudu Mungu tu”, Papa alisisitiza na kusema “mambo mengine ndiyo yana mafao  , lakini yanafaa  ikiwa mimi ninao uwezo wa kuabudu Mungu tu peke yake. Akionesha  namna ya kuweza kuabudu alitoa ushauri ya kwamba “Kuna sala moja ndogo tunayoisali, ya Atukuzwe: Atukuzwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, lakini wakati mwingine tunaisema sala hiyo  kama kasuku, japokuwa sala hiyo ni ya kuabu! Atukuzwe : maana yeke ni ninaabudu baba ; mwana na Roho Mtakatifu. Ni kuabudu kwa njia ya sala na ukimya  mbele ye ukuu wa Mungu, ni kuabudu Yesu ukisema “ wewe tu peke yako , ni wewe uliye mwanzo na mwisho , ni wewe tu ninataka nibaki nawe maisha yangu na daima, kwani ni wewe tu uliye peke yako, kwa kusali hivyo ni wakati ukitafuta namna ya kufukuza yote yanayo kuzuia usiabudu Yesu.

Zoezi la tatu ni la kumfuata Yesu" aliendelea Baba Mtakatifu “ kama isemavyo maneno ya injili ya siku ya Jumatatu , ambapo Bwana aliwaita mitume wa kwanza. Papa alisema hiyo ni kumweka Yesu awe kitovu cha maisha yetu: maisha ya kikristo ni rahisi na kitu rahisi  lakini tunahitaji msaada na neema ya Roho mtakatifu kwasababu aweze kuamsha ndani yetu ile tamaa ya  kumjua , kuabudu  na kumfuata Yesu. Na ndiyo maana sala ya mwanzo wa kuabudu Ekaristi  tunaomba kwa Bwana aweze kutufanya tumjue na kuwa na nguvu ya kutenda  hivyo kila siku ya maisha yetu . Maisha ya kikristo ni rahisi , na wala siyo mahitaji ya kitu ambacho ni cha  kusatajabisha  au kigumu, bali ni kuweka Yesu  mstari wa mbele kwenye uchaguzi wa maisha yetu ya kila siku.Alimalizia akisema Bwana atupatie  neema ya kumjua, kumwabudu na kumfuata Yesu "

Sr Angela Rwezaula.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.